Mkuu wa wilaya ya Same, Kasilda Mgeni ameendelea na ziara ya kikazi katika Tarafa ya Same ambapo ameweza kukagua mradi wa ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari Moipo ambao umegharimu sh. mil.126 na mradi wa Kituo cha Afya cha Tarafa.
Pia DC Kasilda amefanya mkutano wa hadhara katika kata hiyo ya Ruvu ambapo amewasisitiza wazazi kuhakikisha wanapeleka chakula cha mchana ili watoto waweze kupata chakula wakati wakiwa shuleni lengo ni kuondoa utoro, hili kupata ufaulu mzuri kwa watoto wakiwa wanakula vyema shuleni
Aidha, ameelekeza wananchi kuepuka desturi ziziso za kiafrika hususani za kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ubakaji na ulawiti na kuhakikisha wanakemea vitendo hivyo vinavyochochea maadili kuporomoka na kurudisha maendeleo nyuma.
DC Kaslida amewataka wananchi kusimamia miradi yote inayotekelezwa na serikali ili kuweza kuilinda na waendelee kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vya rushwa ndani ya mradi
Kaslida Amewataka wakulima na wafugaji kuendelea kuheshimiana kwa kutoingiza mifungo ndani ya mashamba na wakulima kutolima maeneo ya mifungo kwa kufanya hivyo migogoro ya wakulima na wafugaji itapotea kabisa.
Aidha, amemwelekeza mhandisi kuhakikisha fedha za nyongeza kiasi cha shilingi 30milioni katika ujenzi wa bweni la sekondari Moipo zinakamilisha ujenzi huo ifikapo tarehe 08.04.2023.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇