LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 17, 2023

SHULE 18 ZASHIRIKI MASHINDANO YA AFRICAN OPEN SCHOOL DEBATE






 Mkurugezi wa Shule za Feza Tanzania, Ibrahim Yunus akizungumza na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za binafsi na serikali wakati  akifungua mashindano ya African Open schools Debate champion ambayo yanafanyika kwa muda wa siku tatu ndani ya  Shule ya kimataifa Feza.  


Amesema shule zipatazo 18 zimeshiriki mashindano hayo za serikali na binafsi lengo ni kuwajenga wanafunzi waweze kujiamini kwenye midahalo mikubwa ya kimataifa na ya kitaifa na kuweza kujifunza vitu tofauti ambavyo vinaweza kujenga nchi yetu na kutengeneza ushirikiano bora kwa wanafunzi katika masomo. 


Pia mmoja wa walimu wa Shule ya sekondari ya kondo hiliyopo Tegeta Grace Saware  amesema midahalo hii inawajenga watoto kwa asilimia kubwa sana Mada zinazotolewa ni nzuri ambazo zipo kwenye mitahara yetu ya Elimu ya hapa Tanzania 


Pia ametoa wito kwa serikali kuwaomba kutengeneza programu za midahalo ya shule za serikali katika wilaya, kata, na mkoa kwani zinawajengea uwezo mkubwa wanafunzi kujiamini na kujieleza hata kwenye mithihan yao

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages