Wananchi Engaeuka Monduli wafurahia kituo cha Afya.
MKUU wa wilaya ya Monduli jijini Arusha, Suleiman
Mwenda amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza na kutatua
kero za wananchi.
Mwenda alisema anafanya hivyo kwa sababu Rais Dk.
Samia Suluhu Hassan alitoa fedha nyingi katika idara ya afya kwa lengo la
kuhakikisha wananchi wanapata matibabu karibu na maeneo wanayoishi.
Akizungumza na wananchi jana wakati
alipotembelea mradi wa kituo cha afya kata ya Engaruka wilayani hapo, Mwenda
aliwataka wananchi kuendelea kuiunga mkono serikali kwa sababu inawajali.
‘’ Ndungu zangu Rais Dk. Samia alileta fedha
nyingi sana, hivyo ni wajibu watu kusimamia miradi hii ikamilike kwa wakati na
iwe na samani ya fedha,’’ alisema.
Aidha, alisisitiza kuwa ujenzi unatakiwa
kukamilika haraka kwa sababu Halmashauri hiyo imeshapokea vifaa vyenye thamani
ya sh 400 milioni vitakavyotumika katika kituo hicho cha Afya.
Akisoma taarifa fupi mbele ya mkuu huyo wa wilaya
Kaimu Mganga mkuu wa Hospitali iliyopo katika Halmashauri hiyo, Constantine
Rahi alisema wanaweka nguvu kuhakikisha maagizo ya mkuu huyo wa wilaya yanatimia
kwa wakati.
‘’ Hadi hivi sasa ujenzi wa kituo cha Afya umeishagharimu
kiasi cha sh 188 milioni kukamilisha jengo la upasuaji na maabara, hivyo
ninaamini tutakamilisha kwa wakati,’’ alisema.
Aliwahakikisha wananchi kuwa serikali imewaletea
vifaa vitakavyotumika katika kituo hicho, hivyo wamejipanga kuwahudumia
wananchi kutimiza malengo ya serikali.
Kwa upande wao wananchi waliofurika katika ziara
hiyo wa walimshukuru Dk. Samia kwa sababu amewaletea huduma hiyo karibu.
Joyce Joseph alisema huduma ya afya walilazimika
kuifuata umbali wa kilometa 60 kwenda Mto wa Mbu kutoka katika makazi waliokuwa
wanaishi.
‘’ Ilikua ni adha na azabu kufuta huduma mbali, tunamshukuru
Rasi Samia kutusogezea huduma hii karibu hakika Mungu ndie anaweza kumlipa
badala Rais wetu,’’ alisema.
Mkuu wa wilaya ya Monduli anaendelea na ziara ya
kutembelea takribani kata 18 za wilaya hiyo kusikiliza na kutatua kero za
wananchi.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa ya kuhakikisha falsafa ya Rais Dk. Samia kuwahudumia
wananchi inatimia kikamilifu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇