LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 22, 2023

TANESCO IMEKUJA NA MKOMBOZI MRADI WA GRIDI IMARA



Na Richard Mwaikenda, Dodoma

 Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kutambua matatizo ya umeme yaliyopo nchini imekuja na mradi wa Gridi Imara ambapo katika bajeti ya mwaka huu imetengewa shilingi bilioni 500 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wake.

 Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Martin Mwambene amebainisha hilo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya shirika hilo Februari 22, 2023 jijini Dodoma.


 Amesema mradi wa Grid Imara utajumuisha ununuzi wa mashine umba 6000,mita laki 7 za umeme, nguzo 380,000,ununuzi na ufungaji wa nyaya zenye urefu wa km 40,000, ujenzi wa njia za kusafirisha umeme mkubwa takribani kilomita 948 na ujenzi wa vituo 14 vya kupooza umeme. 

 

Kaimu Mkurugenzi huyo amezungumzia pia maendeleo ya ujenzi katika Bwawa la Mwalimu NYerere kuwa upo katika asislimia 88 na zoezi la uwekaji maji limefikia mita za ujazo 133 kutoka usawa wa bahari.


 Mwambene amesema kuwa hadi kufikia mwaka 2025 Shirika hilo litakuwa limefikia malengo ya uzalishaji wa Megawati 5000,kutokana na miradi kadhaa ambayo inachangia kuongeza uzalishaji wa umeme katika gridi ya taifa kila mwaka.



Amesema kuwa kwa sasa shirika hilo lina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 1,820,wakati mitambo iliyopo ina uwezo wa kuzalisha megawati 1,300 pekee. 

 

 "TANESCO inafanya miradi kadhaa ambayo inasaidia kuongeza kiwango cha umeme katika Gridi ya Taifa kila mwaka ambapo malengo ni kufikia Megawati 5000 ifikapo 2025,"amesema Mwambene 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages