LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 22, 2023

KUNA ENEO LA KUFANYIA BIASHARA LIMETENGWA PANGANI ASEMA MSEMAJI WA SHIUMA MKOA PWANI DISMAS LYASSA

Msemaji wa Shirikiko la Wafanyabiashara wadogo na wa kati Mkoa wa Pwani (SHIUMA) ndugu Dismas Lyassa amewataka machinga katika Kata Pangani kuacha kuwa na hofu juu ya wapi watafanyia biashara zao, akisema kuwa kumekuwa na mazungumzo mazuri baina ya SHIUMA na ofisi ya Mkoa wa Pwani ambayo yamehitimisha kwamba kuna eneo linatengwa kwa ajili ya machinga katika Kata Pangani.

"Nimekuwa nikisikia baadhi ya wajasiriamali wakiuliza hivi sisi wakazi wa Pangani kweli tuna eneo au la, niwwahakikishie kwamba tumekuwa na mazungumzo na ofisi ya Mkuu wa Mkoa, tunaipongeza sana ni ofisi sikivu, tumeshahakikishIwa kwamba katika Kata ya Pangani liko eneo maalum kwa ajili yetu machinga," anasema Dismas Lyassa.

Kulingana na ndugu Lyassa, azma ni kuhakikisha Kata ya Pangani inakuwa na eneo maalum kwa ajili ya wafanyabiashara, eneo ambalo litawapa uhuru wafanyabiashara kuendesha shughuli zao vizuri na kwa mafanikio.

"Hivi karibuni pia tumekuwa na mazunguma na benki ya CRDB kuangalia namna gani wanaweza kuwasaidia machinga bila usumbufu hasa mikopo nafuu, kwa ujumla ziko fursa nyingi kwa machinga wa mkoa wa Pwani nzima, wakati ukifika tutapita kata kwa kata au wilaya kwa wilaya na kueleza kwa kina namna jamii hasa machinga kwa maana ya wafanyabiashara ndogo na kati wanavyoweza kunufaika kwa fursa hizo," anasisitiza Lyassa.

Lyassa anawaomba wachinga kufanya biashara rasmni ikiwamo kufuata taratibu za kuwa na vitambulisho vya machinga au taratibu nyinginezo za uendeshaji masuala ya ujasiriamali kwani ndio inakuwa rahisi kupata mikopo rafiki.

"Wengi wamekuwa wakiuliza vipi kuhusu vitambulisho vya ujasiriamali, lakini ukweli ni kwamba vitambulisho vipo na vinaendelea kutolewa, tena vitambulisho vinavyotolewa sasa vimeboreshwa zaidi, ni vizuri wajasiriamali kupendelea kutembelea ofisi za serikali zilizoko karibu hasa kuwaona maofisa maendeleo kwa ufafanuzi juu ya vitambulisho hivyo," anasisitiza.

"Wote wanaofanya shughuli mbalimbali za kiuchumi waendesha shughuli zao katika mfumo rasmi, mfano kama ni madereva wa bodaboda wajiunge kwenye vikundi, ziko bodaboda nyingi za kukopa, pia ziko fedha na aina nyingine ya uwezeshaji, lakini ili walengwa wanufaike ni lazima wawe rasmi," anasema.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages