LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 12, 2023

SUBIRA MGALU APONGEZA MAFANIKIO KATIKA SEKTA YA FEDHA 2022+video

Mbunge wa Viti Maalumu, Subira Mgalu amepongeza mafanikio katika sekta ya fedha nchini ambayo haijawahi tokea tangu tupate Uhuru 1961.

Aidha, Mgalu ameiomba benki hiyo katika bunge lijalo waende kuwapiga msasa wabunge wanawake kuhusu fursa hizo za mikopo.

Ametoa pongezi hizo alipokuwa akitoa shukrani wakati wa semina fupi iliyotolewa na Benki ya NMB kwa watumishi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT TAIFA) Makao Makuu ya umoja huo jijini Dodoma Februari 10, 2023.

Semina hiyo ilikuwa inahusu fursa za mikopo yenye riba na masharti nafuu inayotolewa na benki hiyo.


Mbunge wa Viti Maalumu, Subira Mgalu akimshukuru Mkuu wa Idara ya Biashara ya Serikali NMB Makao Makuu, Vick Bishubo kwa semina waliyotoa kwa UWT. Katikati ni Katibu Mkuu wa UWT Taifa, Philis Nyimbi.
Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda (kulia) akipongezana na Mkuu wa Idara ya Biashara ya Serikali NMB Makao Makuu, Vick Bishubo baada ya  semina hiyo kumalizika.
Viongozi na watumishi wa UWT wakiwa katika semina hiyo.
Mgalu (katikati) akiwa na mbunge mwenzie Neema Rugangira (kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu UWT Taifa Tanzania Bara, Riziki Kingwande.
Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda (katikati) akiwa na viongozi wa wengine wa UWT Taifa, wabunge na viongozi wa NMB.
Katibu Mkuu wa UWT Taifa, Philis Nyimbi, akiagana na Mkuu wa Idara ya Biashara ya Serikali NMB Makao Makuu, Vick Bishubo baada ya  semina hiyo kumalizika.

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video,Mgalu akitoa pongezi na ombi hilo...
 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages