LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 24, 2023

RAIS MSTAAFU JK NCHINI MAREKANI, LEO

 Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe. George W. Bush na Dkt. Condoleezza Rice, Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu wa Marekani, wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Miaka 20 ya Mpango wa Dharura wa Rais wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR), Jijini Washington DC Marekani leo.


Katika kuadhimisha miaka hiyo 20 ya mafanikio ya PEPFAR, licha ya kwamba Programu hiyo inatekelezwa katika nchi mbalimbali Afrika na Asia, Taasisi ya George Bush Foundation wameamua kumualika Dkt. Kikwete kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuifanya Program hiyo kuwa na mafanikio. 


Tanzania imekua ni nchi ya kupigiwa mfano kwa namna walivyofanya jitihada za kupambana na ugonjwa wa UKIMWI kwa jitihada zao wenyewe kama nchi na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kimataifa kama vile PEPFAR.



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages