Shirika la Omuka Hub na Small Media la Uingereza wamezindua programu ya Haki za Kidijitali kwa kuwapatia mafunzo ya uelewa juu ya jambo hilo baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma Februari 5, 2023.
Semina ya hiyo kwa wabunge ilikuwa inahusu Tathmini ya Umoja wa Kimataifa ya Ulimwengu ya Hali ya Haki za Binadamu kwa Upande wa Haki za Kidijitali.
Wabunge waliohudhulia semina hiyo wameyapongeza mashirika hayo kwa kuwaandalia mafunzo hayo, lakini wamempongeza Mwasisi wa Omuka Hub, mbunge mwenzao Neema Rugangira kwa kufanikisha mafunzo hayo.
Catherine Anite kutoka Small Media akiendesha mafunzo hayo kwa wabunge.
Neema akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Matiko.
Wabunge waliohudhuria mafunzo hayo wAkiwa katika picha ya pamoja na waandaji wa semina.
Waandaji wa semina hiyo.
Wabunge wakiwa makini kusikiliza wakati wa semina hiyo.
Mbunge Ester Matiko akichangia jambo wakati wa semina.
Afisa Programu Mwandamizi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Raymond Kanegene akitoa mafunzo kuhusu haki za binadamu na kidijitali.
Mbunge wa Viti Maalumu, Nusrat Hanje akiuliza swali ili kupata uelewa zaidi.
Mbunge wa Viti Maalumu, Tecra Ungele akielezea jinsi wabunge walivyonufaika na semina hiyo na kuzipongeza taasisi zilizoandaa.
Mbunge wa Kiteto, Edward Olekaita akitoa pongezo kwa Omuka Hub kwa kuwaandalia mafunzo hayo na jinsi walivyonufaika nayo..
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, wabunge wakitoa pongezi kwa waandaji pamoja na kuelezea walivyonufaika na maafunzo hayo...
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇