LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 14, 2023

NEEC : ZAIDI YA WATANZANIA 83,000 WAMEPATA AJIRA KWENYE MIRADI YA KIMKAKATI

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa akieleza utekelezaji wa majukumu ya Baraza hilo katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita leo Februari 14, 2023 kwenye ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dodoma.
Wanahabari wakiwajibika wakati wa mkutanmo huo.


Na Richard Mwaikenda, Dodoma


 Zaidi ya Watanzania  83,000 wamepata ajira katika miradi ya kimkakati hapa nchini ambayo kwa hivi sasa Zaidi ya kamp[uni 1,770 za Kitanzanioa  zimepata tenda katika miradi hiyo.

Hilo limebainishwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa wakati wa mkutano na wanahabari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma Februari 14, 2023 alipokuwa akieleza utakelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo.

Aidha,Beng'i amesema Baraza lina majukumu ya kuwezesha kubuni, kupanga, kusimamia, kufuatilia, kutathmini na kuratibu shughuli zote za uwezeshaji wa kiuchumi nchini.

Pia,Baraza linasimamia na kuratibu mifuko na programu za uwezeshaji na kwamba  hadi sasa nchini kuna mifuko zaidi ya 72.

Mifuko inayosimamiwa ni pamoja na  inayotoa mikopo moja kwa moja,  Mfano Women Development Fund, SELF Microfinance, inayotoa dhamana, Mfano PASS Trust, Mfuko wa Nishati Jadidifu na  inayotoa ruzuku, Mfano TASAF, Mfuko wa Misitu Tanzania (TAFF).

Lakini pia Beng'i amesema NEEC inasimamia programu za uwezeshaji (Viwanda Scheme) hapa wafanyabiashara wenye viwanda vidogo na vya kati hukopeshwa.

"NEEC hadi sasa imewezesha kuwapatia ya zaidi ya Shilingi Bilioni 3.5 wafanyabiashara wenye viwanda vya kati na vidogo katika miradi 62 kwenye mikoa 12 nchini,"amesema.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages