LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 26, 2023

MWAJABU MBWAMBO: REJESHENI MIKOPO YA HALMASHAURI KWA WAKATI MSIKWAMISHE NIA NJEMA YA RAIS SAMIA

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Masaki
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo, amewahimiza  Wanawake, Vijana na Wenye ulemavu kuhakikisha wanapopewa mikopo inayotolewa na  Halmashauri, wanarejesha kwa wakati kwa kuwa wasipofanya hivyo wanakwaza nia njema ya Rais Samia Suluhu Hassan kuyakomboa makundi hayo kiuchumi.

Amesema, nia ya Rais Samia ni kuhakikisha Wanawake, Vijana na wenye ulemavu wananufaika wote na mikopo hiyo inayotolewa na Serikali kupitia Halmashauri zote nchini, kwa hiyo wanaipata wasiporejesha kwa wakati wanasababisha wenzao wengine kukosa.

Aliyasema hayo jana, akizungumza na Viongozi na Wanachama wa UWT, Tawi la Masaki Kata ya Msasani, katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa UWT tawi hilo, ambako alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Sophia Mjema.

"Najua ninyi Kina mama mnampenda Sana Mwenyekiti wetu wa CCM Rais Samia, sasa ili mdhihirishe upendo huo, hakikisheni kila mnapopata mikopo hii anayotoa mnarejesha kwa wakati, maana msipofanya hivyo mnakwamisha juhudi zake za kuwakomboa kiuchumi, Vijana na Wenye ulemavu.

Tazama Afisa Maendeleo ametuambia hapa kwamba katika kipindi cha mwaka 2021-22 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni peke yake ilitoa Sh. Bilioni 18. 8 kuwakopesha ninyi Wanawake, Vijana na wenye ulemavu, lakini hadi sasa zaidi ya Sh. Bilioni 11 hazijarejeshwa, sasa katika hali kama hiyo wengine watakopeshwa fedha zipi?", alisema Mwenyekiti Mwajabu.

Aliwataka viongozi katika mkoa wa Dar es Salaam, kuhakikisha wanakuwa wanafuatilia mara kwa mara tena kwa karibu utoaji na urejeshaji wa mikopo hiyo, na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria kwa wale watakaokuwa hawarejeshi.

Mwenyekiti Mwajabu, alisema, moja ya sababu inayokwamisha urejeshaji wa mikopo hasa kwa kina mama na vijana, ni kugeuza matumizi ya mikopo hiyo kufanyia mambo mengine kama kununua mavazi na vipodozi  na kufanyia starehe hasa kwa vijana, badala ya kuanzishia au kuendeleza miradi ya uzalishaji.

Aliwataka pia UWT na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa jumla kujikita katika kubuni na kuanzisha miradi ya kiuchumi ili Chama ndiyo kiwategemee badala ya wao (wanachama) kukitegemea.

"Chama kimesema wazi, kiongozi lazima awe na kazi ya kumwingizia kipato, sasa wengine wanapopata uongozi wanatarajia kwamba humo ndiko watapata pesa, hii siyo sahihi, inatakiwa mnapokuwa katika Jumuiya au Chama muunde makundi ya ujasiriamali ili kila mmoja aweze kujikimu kutokana na miradi hiyo", alisema Mwenyekiti Mwajabu.

Mbali na kuzungumzia mikopo hiyo Mwenyekiti Mwajabu alizungumzia pia haja ya Jamii kuendelea kusimamia maadili ili kuondokana au kupunguza ukatili kwa watoto na kuporomoka kwa maadili hasa kwa vijana.

Katika Mkutano huo uliofanyika Ofisi ya CCM tawi la Masaki, Mwenyekiti Mwajabu ambaye alifuatana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya UWT Taifa Doreen Kahwa, alipokea wanachama wapya 28 wa UWT na kuwakabidhi kadi za Ujoma huo.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo, akizungumza katika Mkutano Mkuu wa UWT Tawi la Masaki, uliofanyika jana, Ofisi ya CCM Tawi la Masaki, katika mkoa huo, jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT tawi hilo Rose Mkisi na kulia ni Mwenyekiti wa UWT Kata ya Msasani Wema Kasuga. (.Picha na Bashir Nkoromo)

Picha za hafla hiyo kuanzia mwanzo👇

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo (wapili kulia) akiwa amepokewa na Viongozi wa UWT tawi la Msaki baada ya kuwasili kushiriki kikao hicho.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo, akiwa amekata utepe kwa ajili ya kuingia kwa mara ya kwanza kwenye Ofisi ya CCM tawi la Masaki, kushiriki Kikao hicho cha UWT tawi hilo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo, akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko wa UTT Amis Benedict Raphael (kulia), alipokagua huduma za Taasisi hiyo ya Uwekezaji baada ya kufika kwenye Mkutano huo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo akipata maelezo alipokagua shughuli za Wajasiliamali wliokuwa wakionyesha bidhaa zao, kwenye Mkutano huo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo, akipata maelezo kwa mjasiliamali aliyekuwa akionyesha bidhaa zake kwenye Mkutano huo.

Wanachama wa UWT Kata ya Masaki wakiwa tayari kwenye Mkutano huo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Oysterbay wakiwa kwenye Mkutano huo kwa mwaliko wa UTW Tawi la Masaki. Shule hiyo ndiyo pekee ya Serikali iliyopo Kata ya Msasani. Walialikwa kwa kuwa UWT ni Jumuia ya CCM inayojihusisha na malezi ya Vijana na Watoto.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Oysterbay wakiwa kwenye Mkutano huo kwa mwaliko wa UTW Tawi la Masaki. Shule hiyo ndiyo pekee ya Serikali iliyopo Kata ya Msasani.
Mwenyekiti wa UWT Tawi la Masaki Rose Mkisi, akifungua Mkutano huo. Kushoto ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya UWT Taifa Doreen Kahwa na Kulia ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Mwajabu Mbwambo akikabidhi katoni za taulo za kike kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Oysterbay, ambazo zimetolewa na UWT Tawi la Masaki. Kushoto ni Mwalimu wa Shule hiyo  Saimon Mwaifei.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Mwajabu Mbwambo akikabidhi madaftari kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum wa shule ya Sekondari Oysterbay.
Mwenyekiti wa CCM Tawi la Masaki Raphael Kamana akizungumza baada ya kupewa nafasi ya kusalimia.
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Msasani Wema Kasuga, akimkaribisha kuzungumza.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya UWT Taifa Doreen Kahwa akizungumza baada ya Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, kumtambulisha.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa UWT, uliofanyika leo katika Ofisi ya CCM Tawi la Masaki, Kata ya Msasani, katika mkoa huo, leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT tawi la Masaki Rose Mkisi na kulia ni Mwenyekiti wa UWT Kata ya Msasani Wema Kasuga.
Baada ya hotuba, Wajumbe wakalipuka kumshangilia Mwenyekiti Mwajabu.
Wajumbe wakiendelea kumpongeza Mwenyekiti Mwajabu kwa hotuba yake.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo akizungumza jambo na Mwenyekiti wa UWT tawi la Masaki Rose Mkisi.
Mwenyekiti wa UWT Tawi la Masaki akizungumza na kisha kuitisha zawadi ili akabidhiwe Mwenyekiti Mwajabu.
Mwenyekiti Mwajabu akikabidhiwa zawadi ya zulia.
Kisha akapewa zawadi ya sare ya UWT wa Masaki.
Na Doreen Kahwa pia akapewa zawadi ya sare ya UWT Masaki.
Mwenyekiti Mwajabu akashukuru kwa zawadi alizopewa yeye na wenzake.
Katibu wa CCM Kata ya Msasani Badili Mangula akizungumza baada ya kupewa nafasi ya kutoa shukurani.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Msasani pia akapata nafasi ya kuzungumza neno la shukurani.

Mwenyekiti wa UWT tawi la Masaki  akafunga rasmi Kikao.
Mwenyekiti Mwajabu akiwa katika picha ya kumbukumbu na baadhi ya Viongozi, mwishoni ya kikao hicho.
Wanafunzi wa Sekondari ya Oysterbay wakila chakula.
Mwenyekiti Mwajabu na baadhi ya viongozi wakiwa katika Picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari. Oysterbay mwishoni mwa Kikao hicho. Katika Kikao hicho Mwajabu alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi  Sophia Mjema.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages