Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo amesisitiza kuwa mfumumuko wa bei siyo tatizo lililoletwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. Samia Suluhu Hassan bali ni tatizo la Dunia nzima.
Amesema kutokana na ukweli huo wasioitakia Tanzania wasijaribu kulitumia tatizo hilo la mfumuko wa bei kuligeuza ndiyo kirungu cha kumpigia Rais Dk. Samia kwa kuwa licha ya kuwa kubwa lakini amejitahidi kupambana nalo kwa kadri inavyowezekana.
"Ninyi wenyewe mmeona, Rais Dk. Samia katika kukabiliana na mfumuko wa bei ameweka ruzuku kwenye mafuta, hii imeleta nafuu sana ya bei ya bidhaa hii, mafuta ndiyo yanayoendesha mitambo ya uzalishaji na usafirishaji, kama Mama asingeweka ruzuku bei ya mafuta ingekuwaje wakati huu?", alisema na kuhoji Mwenyekiti Mwajabu.
Mwenyekiti Mwajabu ameyasema hayo, jana, wakati akizungumza katika Kikao cha Baraza la UWT Kata ya Somangila, Wilaya ya Kigamboni, uliofanyika katika Ukumbi wa Arema, na yeye kuwa mgeni rasmi na kuhudhuriwa na Viongozi wa CCM, UVCCM wa Kata hiyo na Wabunge na Madiwani wa Viti Maalum Kgamboni.
Amesema, mbali na Tanzania nchi mbalimbali duniani yakiwemo Mataifa makubwa kama Marekani kipindi hiki wanahangaika kukabiliana na mfumuko huo wa bei ambao kwa sehemu kubwa umetokana na athari za ugonjwa wa Uviko-19 ulioikumba dunia miaka michache iliyopita.
Kutokana na hali hiyo Mwenyekiti Mwajabu amewataka Viongozi wa UWT na wana CCM katika Kata hiyo kuhakikisha wanaeleza wananchi ukweli kuhusu Rais Samia anavyokabiliana na mfumuko huo wa bei. na pia kueleza kwa takwimu mafanikio yaliyopatikana hadi sasa chini ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.
Amesema kwa upande wa Wilaya ya Kigamboni ilimo Kata ya Somangila, yapo mengi mazuri yamefanywa na Rais Dk. Samia, hasa nayaohusu Wanawake na watoto ikiwemo kujengwa Kituo cha Afya Mbutu Kichangani Somangira, Mradi wa maji kwa kusambazwa mabomba Kata ya Kisarawe II.
Kuhusu Uhai wa Chama na UWT katika Kata hiyo, Mwenyekiti Mwajabu aliwahimiza Viongozi wa CCM na UWT, kuhakikisha wanakuwa na 'data' sahihi za idadi za Wanachama ikiwa ni njia mojawapo ya kujipanga kwa ajili ya Uchaguzi 2024/2025.
Aliwakumbusha pia kwamba katika kujipanga huko waandae mikakati madhubuti ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wanawake na Mabinti wenye sifa kwa kuwashawishi kuomba nafasi za uongozi muda ukifika, badala ya wanawake wao kwa wao kuvunjana nguvu mwenzao anapoonyesha nia ya kuomba uongozi.
Kuhusu ukatili wa kijinsia na mmonyoko wa wa maadili, Mwenyekiti Mwajabu aliwakumbusha suala la kupinga na kukemea ukatili huo ambao alisema bado upo katika jamii akisisitiza pia elimu kutolewa katika familia, akibainisha kuwa umekuwa ukifanywa zaidi na ndugu kwa ndugu.
Amesema ili kukabiliana na mmomonyoko wa maadili Wanawake wahakikishe wanatekeleza jukumu lao kubwa la msingi ambalo ni malezi ya familia japokuwa na wanaume wanahusika katika jukumu hilo.
Katika Kikao hicho Mwenyekiti Mwajabu alipokea wanachama wapya 118 wa UWT kwa kuwapatia kadi za Uanachama.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo akizungumza katika Kikao cha Baraza la UWT Kata ya Somangila, Wilaya ya Kigamboni, jana. Kula ni Katibu wa UWT Somangila Kaiffa Ali na kushoto ni Diwani wa Viti Maalum Kigamboni Elizabeth Kimambo (Lizzy).
Picha zaidi za mtirirko wa tukio, mwanzo hadi mwisho👇
Diwani wa Viti Maalum Kata ya Somangila Elizabeth Kimambo (Lizzy) -kushoto akiwasili ukumbini huku akisindikizwa na Katibu Kaiffa aliyempokea.Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo akiingia ukumbini huku akisindikizwa na baadhi ya viongozi wa UWT Somangila waliompokea.Wajumbea wa Baraza la UWT Somangila wakiserebuka muziki, kumlaki Mwenyekiti Mwajabu Mbwambo ukumbini.Mwenyekiti Mbwambo (wapili kulia) akiwa na baadhi ya viongozi baada ya kuwasili meza kuu.Mwenyekiti Mwajambu akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili ukumbini. "Haya Katibu ratiba ipoje"? akasema Mwenyekiti Mwajabu kumuuliza Katibu Kaiffa (kulia)
"Karibu Karibu Mwenyekiti wetu", akasema MC Sauda Hemed.
Katibu wa UVCCM Kata ya Somangila Asha Abdallah akifanya dua ya Kiislam kubariki Kikao kabla hakijaanza.Mjumbe wa Baraza la UWT Somangila akifanya maombi kabla ya kikao kuanza.Kaimu Mwenyekiti wa Kikao hicho, Katibu wa UWT Somangila Kaiffa akifungua Kikao na kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM Somangila kuzungumza. Mwenyekiti wa CCM kata ya Somangila akizungumza."Oyeeee", wajumbe wakishangilia ukumbini.Msoma risala akakabidhi risala hiyo kwa Mwenyekiti Mwajabu, baada ya kuisoma.Mwenyekiti Mwajabu akiongoza kumtuza msoma utenzi Moza Ally.Mara Moza noti za kutuzwa zivinjari mbele yake huku akiendelea kughani utenzi wake.Kaimu Mwenyekiti wa Kikao hicho Katibu Kaiffa kazungumza na kumkaribisha Mwenyekiti Mwajabu kukabidhi kadi baadhi ya wanachama wapya wa UWT 118 kwa naiaba ya wenzao.Katibu wa UVCCM Kata ya Somangila Asha Abdallah akapokea yake.
Na huyu pia akakabidhiwa yake.Waliokabidhiwa kadi wakala kiapo.Diwani Lizzy akapata nafasi ya kusalimia na kuzungumza machache.
Kisha Mwenyekiti Mwajabu akasimama na kutoa cheche katika hotuba yake. |
Kabla hajaketi papo hapo akapewa zawadi ya Keki muruwa. Anayemkabidhi ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Amina Heri.
Zabibu Urassa akitoa shukrani kwa niaba ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Abubakar Ally Abubakar ambaye hakuwepo lakini alichangia kufanikisha Kikao hicho. Amina ni Mkurugenzi wa Boka Pharmacy ya Kigamboni.
Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji UWT Wilaya ya Kigamboni Hawa ramadhani pia akatoa shukrani kwa mgeni rasmi kwa niaba ya UWT Somangila.
"Mwenzangu Hongera kwa shughuli ya leo, ila sasa inabidi mkaze buti zaidi, maana hili la kuwa Wanachama mfu wengi mnatakiwa mlifanyie kazi zaidi, mjitahidi muwe na orodha sahihi ya wanachama msijekuwa na orodha feki..." akasema Mwenyekiti Mwajabu kumwambia Katibu Kaiffa.
©Feb. 2023 CCM Blog/Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇