Na Fredy Mgunda, Nachingwea.
MKUU
wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amewataka viongozi wa
serikali kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali wanatakiwa kuwatumikia
wananchi wa Nachingwea.
Akizungumza
wakati wa ziara ya kijiji kwa kijiji yenye kauli mbiu isemayo
ulipo nipo sema kweli sio majungu ya ,Moyo alisema kuwa hataki kusikia
habari za mchakato kwenye utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo ya
serikali.
Moyo
aliwataka viongozi kutatua changamoto na kero za wananchi kuanzia ngazi
ya kitongoji hadi wilaya hivyo kama kutakuwa na kiongozi hataendana na
kasi ya serikali ya awamu ya sita basi akae pembeni awapishe wengine
wenye uwezo wa kufanya kazi kwa kasi ya serikali ya awamu ya sita.
Akiongea
na wananchi wa kata ya Mbondo alitoa siku saba kwa uongozi wa
Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kuhakikisha wanawapa wazee kadi za
matibabu kama ambavyo serikali ya awamu ya sita inavyotaka.
Moyo
aliwataka viongozi wa TARURA kuwasimamia vilivyo wakandarasi wote ambao
wamepewe kazi ya ujenzi wa barabara katika wilaya hiyo ili zijengwe kwa
kiwango kinachotakiwa.
Aidha
Moyo alimtaka Injinia wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea
kuhakikisha miradi yote inajengwa kulingana na thamani ya fedha ambazo
zimetolewa na serikali kuu pamoja na Halmashauri kwa faida ya Taifa na
Wananchi wote.
Moyo
alimazia kwa kuwataka wananchi wa wilaya hiyo kuwa walinzi wa amani ili
kuondoa vurugu na migogoro mbalimbali ambayo imekuwa inahatarisha amani
Taifa
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Injinia
Chionda Kawawa alisema kuwa wamepokea maagizo yote yaliyotolewa na mkuu
wa wilaya ya Nachingwea na watayafanyia kazi kwa faida ya wananchi wa
wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kata ya Mbondo wakati wa uzinduzi wa ziara ya kijiji kwa kijiji yenye kauli mbiu isemayo ulipo nipo toa kero yako sio majungu
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kata ya Mbondo wakati wa uzinduzi wa ziara ya kijiji kwa kijiji yenye kauli mbiu isemayo ulipo nipo toa kero yako sio majungu
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kata ya Mbondo wakati wa uzinduzi wa ziara ya kijiji kwa kijiji yenye kauli mbiu isemayo ulipo nipo toa kero yako sio majungu.



No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇