LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 19, 2023

WANNE MBARONI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI KAGERA.

                                              

Kamanda Msaidizi wa uhifadhi na mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ibanda-Kyerwa Fredrick Mofulu akizungumzia tukio hilo. 
Sehemu ya nyara za Serikali zilizokamatwa.


Na Lydia Lugakila,  Bukoba.

Jeshi la uhifadhi Wanyamapori na Misitu kwa kutumia kikosi cha  Askari wa Hifadhi za  Taifa za Ibanda- Kyerwa na Rumanyika- Karagwe wamefanikiwa kuwakamata watu(4) wakiwa na nyara za Serikali pamoja na Siraha za kienyeji ambazo hutumika kuua Wanyamapori.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za  kituo cha Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera Februari 19,2023 Kamishna Msaidizi wa uhifadhi ambaye pia ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ibanda- Kyerwa Fredrick M. Mofulu amesema kuwa  watu hao wanne wamekamatwa mnamo Februari 13, 2023 majira ya saa tatu usiku walipata taarifa za Kiintelijensia juu ya uwepo wa mtandao wa watu wanaojihusisha na ujangili wa Wanyamapori pamoja na biashara ya nyara za Serikali.

Kamanda  Mofulu  amezitaja Nyara za Serikali zilizokamatwa kuwa ni pamoja na Meno mawili ya Tembo, Ngozi ya Fisi, kichwa cha Fisi, vipande vitatu vya ngozi ya nyati na mkia mmoja wa nyati pamoja na ngozi ya swala pala.

Aidha Majangili hao wamekutwa na Silaha mbili aina ya Gobore pamoja na risasi tatu za kienyeji aina ya Gololi ambazo hutumika kwa ajili kuua Wanyamapori.

Ameongeza kuwa tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Muungano na Lusahunga Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera.

Amesema kati ya meno ya tembo yaliyokamatwa jino moja lenye alama ya A lina uzito wa kilogram 4.75 wakati jino la pili lenye alama A1 likiwa na uzito wa kilogram 4.40 

Amewataja waliokamatwa kuhusika katika tukio hilo kuwa ni    Raphael Daudi Lugaira(44) Fikiri Simon Lugaira (43), Majaliwa Isaya Charles (42) na Warwa Buduru Rupilya(45) wote wakazi wa Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera.

Jeshi la uhifadhi Wanyamapori na Misitu linatoa limewataka Watanzania kuacha kabisa kujihusisha vitendo vya ujangili dhidi ya maliasili kwani watakaokaidi watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Hata hivyo kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera ACP William Mwampagale amesema kuwa wamekuwa wakishirikiana na  uhifadhi katika suala zima la operesheni na kuahidi kuwa zitakuwa operesheni endelevu huku akiwataka akitoa wito kwa Wananchi Mkoani humo kuendelea kushirikiana na Wahifadhi ili kuwabaini wanaojihusisha na ujangili wa aina hiyo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages