LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 11, 2023

MKUU WA WILAYA TUKAI APIGA MARUFUKU UNENGULISHA WATOTO KWENYE SHEREHE

 

Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Naitapwaki Tukai akizungumza na mwandishi was habari ofisini kwake.

NA ODACE RWIMO, NZEGA

MKUU wa Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Naitapwaki Tukai amepiga marufuku kutumia watoto wenye umri chini ya miaka 18 kunenguwa kwenye majukwaa na sehemu nyingine za sherehe kwa kuwa kitendo hicho kinakiuka haki za watoto.

Akizungumza na mwandishi wa habari ofisini kwake alisema kutumia watoto kwenye sherehe kama wanenguaji ni mmomonyoko wa maadili pia inashusha morali ya masomo kwa watoto hao kwani hawataweza kufikilia masoma zaidi ya kucheza.

Alisema suala hili kuanzia leo sitopenda kuliona kwenye tukio lolote kwani sheria itafuata mkondo wake kama ni vipaji vya watoto vitapatikana pale panapohitajika kutafta vipaji hivyo na siyo kuwatumia kupendezesha sherehe hilo halikubaliki katika jamii yetu ya kitanzania kuwatumia watoto.

“ Hapa nazungumza kama mzazi ambaye ninawatoto lakini kama mkuu wa wilaya ya Nzega sitokubali kuona watoto wanaharibikiwa kupitia kunenguwa wakati nikiwa hapa Nzega na huu ni ukiukwaji wa haki za mtoto sitolikubali ntawalinda kwa nguza zangu zote sotorudi nyuma lazima watoto tuwaache waweza elimu”alisema Tukai.

Katika hatua nyingine akizungumzia suala la miradi ya maendeleo alisema amelizishwa na kasi ya utekelezaji hasa mradi mkubwa wa kitaifa wa Bomba la mafuta na ujengaji wa Kambi Jeshi la kujenga taifa ambao pia unaendelea vizuri.

Alisema miradi hii ya kitaifa inapotekelezwa kwa weredi ni jambo la kujipongeza hasa kama wilaya  nitafuatilia hatua kwa hatua namna inavyotekelezwa miradi hii kwani ni fedha ya serikali ambayo inatumika kutekeleza miradi hii.

Alisema kwa upande wa elimu ya awali wanafunzi waliojiandikisha wamefikia asilimia 83 ambapo anatarajia kuona uandikishwaji wa watoto ukienda zaidi hadi kufikia asilimia 100 ifikapo mwezi march mwaka huu.

“Tayari nimeisha ongea na watendaji wa kata na vijiji ikiwa ni pamoja na madiwani kuwaelimisha wazazi juu ya umuhimu wa kuwapeleka watoto shuleni kwani ni haki yao ya msingi na elimu inatolewa bure bila gharama yoyote.

Alisema serikali ya awamu ya sita Chini ya Dr.Samia suluhu Hassan imejikita kuahikiksha watoto wanapata elimu bure kuanzia darasa la awali mpaka kidato cha sita jambo hili  ni la kumpongeza rais na kumuunga mkono kwa nguvu zote.

Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia suluhu Hassani amekuwa kiongozi wa kuigwa ndani ya Bara la Afrika na Dunia nzima kwa ujumla kwa namna ambavyo anapambana kuliendeleza taifa letu na kuleta mshikamano na utulivu  na amani nchini.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages