LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 11, 2023

CHATANDA AWATAKA WANAWAKE KUACHANA NA MIKOPO UJINGA HAUISHI, KAUSHA DAMU KOPENI NMB+video

 


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT TAIFA), Mary Chatanda amewataka wanawake kuachana kabisa na mikopo ya ujinga hauishi na kausha damu.inayowatia umaskini, bali amewashauri kwenda kukopa Benki ya NMB yenye riba na masharti nafuu.

Ametoa ushauri huo mbele ya watumishi wa UWT na wafanyakazi wa NMB waliokwenda Makao Makuu ya umoja huo jijini Dodoma Februari 10, 2023 kuupongeza uongozi mpya wa UWT na kutoa somo kuhusu mikopo mbalimbali inayowagusa wanawake.

Mkuu wa Idara ya Biashara ya Serikali, NMB Makao Makuu, Vick Bishubo akifafanua kuhusu unafuu wa mikopo inayotolewa na benki hiyo.
Kaimu Meneja wa  Benki ya NMB, Kanda ya Kati,  Amos Mubusi akitoa somo kuhusu mikopo mbalimbali inayotolewa  na benki hiyo.
Wabunge wanawake wakihudhuria kikao hicho. Kushoto ni Neema Rugangira, Subira Mgalu na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT Tanzania Bara, Riziki Kingwande.
Watumishi wa UWT wakisikiliza kwa makini wakati somo hilo likitolewa na NMB.



Bishubo akiagana na mbunge Subira Mgalu.
Chatanda akiagana na Bishubo wa NMB.


PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Chatanda akitoa ushauri wake huo....


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages