LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 27, 2023

IRUWASA YAVUKA LENGO LA ILANI YA CCM, WANANCHI IRINGA WAPATA HUDUMA YA MAJI SAA 23 KWA SIKU


 MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA)imefanikiwa  kuvuka lengo la Sera ya Maji na Ilani ya Chama Tawala Cha Mapinduzi (CCM) ya kutoa huduma ya usambazaji maji kwa mji wa Iringa na maeneo ya pembezoni inayowafikia wakazi hao kwa asilimia 97.


IRUWASA imefanikiwa kuhakikisha huduma ya maji Mjini Iringa na maeneo ya pembezoni inapatikana kwa wastani wa saa 23 kwa siku.


Mafanikio hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendahi wa IRUWASA, Mhandisi David Pallangyo wakati wa mkutano na vyombo vya habari wa kuelelezea utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO, jijini Dodoma Februari 27, 2023.


Mhandisi Pallangyo ametaja mafanikio mengine kuwa ni; kuongeza ukusanyaji maduhuli kwa huduma zilizotolewa kutoka wastani wa Shilingi milioni 770 mwaka 2020 kwa mwezi hadi Shilingi milioni 860 kwa mwaka 2023.


Idadi ya wateja/maunganisho ya majisafi imeongezeka kutoka 28,133 mwaka 2020 hadi 40,549 Desemba, 2022.


Na kwa upande wa eneo la TEHAMA, Pallangyo amesema IRUWASA imefanikiwa kwa kufunga mita za malipo kabla kwa wateja 6,752 na kuwa Mamlaka inayoongoza nchini kwa kufunga mita nyingi za maji za malipo kabla.


Aidha Mhandisi Pallangyo amesema kuwa tangu mwezi Machi, 2016 Mamlaka ilianza kuzifungia mita za malipo ya kabla Taasisi za Serikali na wateja wa kawaida na wafanyabiashara ili kudhibiti ongezeko la madeni.


"Mnamo mwezi Desemba, 2022, IRUWASA ilikamilisha utekelezaji mradi wa kusambaza maji kwenye maeneo ya pembezoni mwa mji wa Iringa yaliyo kwenye kata za Mseke, Kalenga na Kiwele kwa gharama ya Shilingi bilioni 1,8," amesema Pallangyo. 


Mbali ya wananchi wapatao 12,930 wanaonufaika na mradi huu, Taasisi mbalimbali kama vile shule, hospitali, vyuo na maeneo ya biashara zitanufaika pia.


No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages