Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo
Tunaishukuru Serikali kutupatia Tsh Milioni 250 kwa ajili ya kujenga miundombinu ya maji ya bomba kati ya vijiji vya Makojo na Chimati.
Maji ya Kijiji cha Chimati yatatoka kwenye TENKI LA UJAZO WA LITA LAKI MOJA (lita 100,000) lililojengwa Kijijini Makojo, na tayari maji ya bomba yanatumika hapo Makojo.
Chanzo cha maji hayo ni kutoka Ziwani Chitare. Tenki la Kijijini Chitare lina ujazo wa LITA 75,000.
Tuendelee kutunza vizuri miundombinu ya uzalishaji na usambazaji wa maji ya bomba kwenye vijiji vyetu.
Taarifa kuhusu matengenezo: Kwa muda wa takribani siku 5, RUWASA imekunya kwenye matengenezo na uboreshaji wa miundombinu ya maji ya bomba vijijini mwetu.
Hadi leo hii maji ya bomba yameanza kupatikana tena baada ya matengenezo kukamilika kwenye vijiji vya:
Wanyere, Mikuyu, Nyambono, Saragana, Kanderema, Bugoji na Kaburabura
RUWASA wanapongezwa kwa kazi nzuri za kuhakikisha maji yanapatikana vijijini mwetu. Wako kazini hata kwa siku za Jumamosi na Jumapili!
Musoma Vijijini tunaendelea kutoa shukrani nyingi sana kwa Serikali yetu inayoongozwa na Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kusambaza maji ya bomba (safi & salama) vijijini mwetu.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumapili, 8.1.2023
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇