Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Mpawe Tutuba kuwa Gavana mpya wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Taarifa iliyotolewa na Ikulu Jijini Dodoma, Januari 7, 2023 usiku wa kuamkia leo Januari 8, 2023, imesema Tutuba anachukua nafasi ya Prof. Florens Luoga ambaye amemaliza muda wake.
Taarifa hiyo mesema, wakati huohuo Rais amemteua aliyekuwa Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Mwenyekiti Bodi ya Kampuni ya Uendeshaji Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO) Dk. Natu El- Maamry Mwamba kuwa Katibu Mkuu Wizara hiyo ya Fedha na Mipango akichukua nafasi ya Tutuba.
"Teuzi hizi zinaanza mara moja", imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus.
Taarifa ya Ikulu hii hapo👇
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇