Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi leo amefungua Hospitali ya Kisasa ya Kitogani Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.
Ufunguaji huo umeambatana na kufungwa kwa vifaa tiba vipya, Gari la kubebea wagonjwa na sasa hospitali hiyo ipo tayari kutoa huduma zikiwemo za wagonjwa wa nje(OPD), Mama na Mtoto, kliniki za Pua, Koo, Masikio, Macho, Magonjwa yasio ya kuambukiza kama Sukari na shinikizo la damu.
Huduma zingine ni za dawa(pharmacy), Wagonjwa wanaolazwa Wodi za Watoto, Wajawazito kabla na baada ya kujifungua, Watu wazima Wanawake na Wanaume, wagonjwa wa dharura na ajali, Wagonjwa mahututi(ICU) na watoto njiti.
Pia zipo wodi tatu za wagonjwa wenye mahitaji maalum ya kujitenga(isolation), Theatres mbili za kisasa, huduma za ushauri nasaha na kupiga vita vitendo vya udhalilishaji na huduma za uchunguzi zikiwemo Maabara, Ultrasound, ECG na XRAYS.
Hospitali hiyo pia ina huduma za kisasa za Mfumo wa Tehama zikiwemo huduma za data, sauti na picha zitakazotumika katika kutoa elimu ya afya kwa wagonjwa na wananchi, usajili wa mahudhurio ya wafanyakazi, mifumo ya tahadhari ya moto, Nursing call System na wa kutunza taarifa za wagonjwa kieletroniki(EMR).
Hospitali itawahudumia Wananchi zaidi ya 52,850 wa Wilaya ya Kusini na maeneo jirani,
📆07 Januari 2023,
đź“ŤHospitali ya Wilaya Kitogani,Wilaya ya Kusini ,Mkoa wa Kusini Unguja.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇