Na Salma Amour, Tanga
Shirika la BORDA linatarajia kutoa Sh. Milioni 246 kwa ajili ya Ujenzi wa Mradi wa Mfumo mpya wa Kupokea, Kuchakata na Kutibu Maji Taka katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe mkoani hapa.
Utekelezaji wa Ujenzi wa Mradi huo ulitangazwa Januari 10, Mwaka huu na Kamati ya Mipango Miji na Mazingira na Uongozi wa Shirika la Maji Safi na Usafi wa Mazingira Korogwe (KUWASA) walipotembelea Kata ya Bagamoyo kwa ajili ya ukaguzi wa eneo la mradi.
Akizungumza, Msimamizi wa Mradi huo Mhandisi wa KUWASA Michael Ntulo, alisema, mradi utaambatana na upatikanaji wa Gati na Guta la kubebea Maji Taka kutoka kwa mwananchi kwa gharama nafuu Ili kupunguza gharama za uchukuzi ukilinganisha na zinazotumika Sasa.
" Kwetu ni jambo jema sana, Mradi huu utakapokamilika licha ya kutunza mazingira pia utasaidia kutoa ajira kwa Wananchi", alisema.
Kwa upande Wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe Rahel Muhando aliesemaeza Ujenzi wa Mfumo wa Kisasa wa Maji Taka katika Mji wa Korogwe ni jambo jema litakaloleta manufaa na Mradi huu utakuwa na tija kwa Wananchi.
"Mimi natoa baraka zote kwa ajili ya utekelezi wa mradi huu, lakini pia utekelezwaji wa ujenzi huo utasaidia mfumo wa kuchakata na kutibu maji taka katika Halmashauri ya mji wa korogwe
Katika hatua nyingine, diwani wa Kata Ya Manundu Rajabu Mzige, ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira ametoa shukrani kwa niaba ya madiwani wenzake na wataalamu wote wa halmashauri ya mji wa korogwe kwa shirika la BORDA kwa kuwapatia mradi huo wa ujenzi wa mfumo wa kisasa wa maji Taka.
"Kwa niaba ya Madiwani wenzangu, pamoja na Wataalamu wote wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe tunatoa shukrani kwa Shirika la BORDA kwa kutupatia Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Kisasa wa Maji Taka, Mradi tumeupokea na tuko tayari kwa utekelezaji wake” . Diwani Rajabu Mzige.
Kamati ya mipango miji na mazingira katika mji wa korogwe ikiwa na viongozi wa KUWASA (Korogwe Urban Water Supply), walipotembelea eneo la Bagamoyo unapotarajiwa kutekeleza mradi huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇