LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 28, 2023

MWENYEKITI UVCCM TABORA AWATAKA VIJANA KUTUMIA MUDA KWA MAENDELEO

Mwenyekiti wa umoja wa vijana Mkoa wa Tabora Kelven Mpiwa akizungumza na wajumbe wa baraza la vijana (hawapo pichani)
Na Odace Rwimo,Tabora
VIJANA wametakiwa kutumia muda wao wa kazi katika kufikilia masuala ya msingi na yenye tija kwa Taifa letu hasa katika kujikwamua kichumi na kujiletea maendeleo makubwa yatakayosaidia Taifa letu kwa wakati huu na ujao.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana CCM Mkoa wa Tabora ndugu Kelvin Mpiwa ameshauri vijana kujikita katika kuzangatia mda ili kuweza kufanikiwa mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja usatwi wa jamii.
Kauli hiyo aliitoa kufuatia  baadhi wa wajumbe wa baraza la vijana mkoa kushindwa kufika kwenye kikao ambacho kilipangwa kufanyika majiara ya saa nne asubuhi na matokeo yake kufanyika mchana.
Huwezi kufanya mambo makubwa kama huwezi kuzingatia mda wako vizuri hivyo nitumie nafasi hii kuwasihi vijana wenzangu kuzangatia mda kwa kila jambo ili tuweze kufanikiwa katika kazi zetu tunazofanya kila wakati.
Mpiwa amewataka viongozi wa wilaya wa jumuiya hiyo kujikita katika kamasaidia Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan  kwa kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni paamoja na kujitolea katika kukijenga chama kwa moyo wa uzalendo.
“Unajua sisi ndio taifa la kesho hivyo viongozi wetu wa kitaifa wanatutegemea katika kufanya mambo makubwa yenye kuleta mabadiliko chanya katika jamii na chama cha mapinduzi kwa ujumla” alisema Mpiwa
Kwa upande wake katibu msaidizi wa CCM Mkoa wa Tabora Mwita Nyarukururu aliseama aliwataka vijana kufanya kazi kwa bidii kwani kazi ndizo zitakazo watambulisha umahili wao kuliko kuwa watu wenye kujiweka kimbelembele bila ya kufanya kazi.
Alisema huwezi kuwa mtu wa kalalamika kwamba ndio kitakusaidia kuonekana unafanya kazi na upate kuteuliwa bali inakubidi ufanye kazi kwa bidii na maarifa kwa kutambua umuhimu wako katika jamii inayokuzunguka kwa kuwasaidia watu wengine  ambao wanakuhitaji katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo.
“Hapa napenda tuweze kuelewana vijana wote wa Mkoa wa Tabora na Tanzania kwa ujumla vijana wengi mmekuwa walalamishi vijeweni bila ya kufanya kazi na agenda yenu kubwa ni kukosoa serikali bila kuzingatia kazi zinazofanyika kila siku jambo ambalo linondoa heshima ya vijana wengi kujitambua na kutambua wajibu wao”aliema Nyarukururu.
Hata hivyo kwa upande wake mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa na Mjumbe wa baraza la vijana mkoa wa Tabora Mosi Bakarri Jengo aliwataka vijana kujikita katika shughuri za uzalishaji mali katika kulijenga taifa letu ambalo limatazama kijna kama shuu wan chi hii.
Alisema ili kama vijana tuweze kuheshimika haina budi kujikita katika kutafuata kazi za uzalishaji mali ikiwa ni pamoja na kilimo ambacho ndio kipaumbele cha Rais wetu mpendwa Dr.Samia Suluhu Hassan ambaye anapenda kuona vijana tunajiajili kwa asilimia kubwa.
Furaha yetu na heshima yetu kama vijana ni uwajibikaji wa hali ya juu na wala siyo kusubilia kuteuliwa katika nyadhifa mbalimbali huko ni kukosa maarifa ya utendaji kazi, hivyo tutumie fursa zinapatikana katika kujikwamua kiuchumi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages