Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati akifungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kilichofanyika leo Januari 30,2023 jijini Dodoma.
- Advertisement -
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Bw.Xavier Daud,akizungumza wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kilichofanyika leo Januari 30,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Usimamizi Maadili kutoka, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Bi.Leila Mavika,akitoa utangulizi wa kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kilichofanyika leo Januari 30,2023 jijini Dodoma.
- Advertisement -
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani),wakati akifungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kilichofanyika leo Januari 30,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Bw.Cosmas Ngangaji,akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) mara baada ya kufungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kilichofanyika leo Januari 30,2023 jijini Dodoma.
- Advertisement -
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama,akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kufungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kilichofanyika leo Januari 30,2023 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kilichofanyika leo Januari 30,2023 jijini Dodoma.
HOTUBA YA MHE. JENISTA JOAKIM MHAGAMA (MB.), WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA KUHUSU MATOKEO YA TAFITI YA HALI YA UZINGATIAJI MAADILI KATIKA UTUMISHI WA UMMA YA MWAKA 2022, KWENYE KIKAO KAZI CHA WADAU WA USIMAMIZI WA MAADILI KATIKA UTUMISHI WA UMMA KATIKA UKUMBI WAKAMBARAGE, DODOMA TAREHE 30 JANUARI, 2023
Dkt. Laurean J. P. Ndumbaro - Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora;
Wakurugenzi wa OR - MUUUB;
Wakurugenzi wa Taasisi Simamizi za Maadili;
Wawakilishi wa Watendaji wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania;
Mahakama na Jeshi la Polisi Tanzania;
Mameneja na Wakurugenzi wa Utawala na
Rasilimaliwatu;
Washiriki wa Kikao Kazi cha Wadau;
Watumishi wa OR - MUUUB mliopo hapa;
Waandishi wa Habari mliopo hapa;
Mabibi na Mabwana.
“Ninawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania”.
Ndugu Viongozi; Awali ya yote napenda kumshukuru
Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema kutujalia uzima
na kutuwezesha kukutana hapa siku ya leo tukiwa na
afya njema tukijiandaa kupokea Matokeo ya Tafiti ya
Hali ya Uadilifu katika Utumishi wa Umma ya
Mwaka 2022.
Kipekee nichukue nafasi hii kuwashukuru kwa utayari
wenu wa kushirikiana na Ofisi hii katika jukumu la
kuimarisha masuala ya Kiutumishi na Utawala Bora
kila inapohitajika. Hii inaonesha dhamira yenu ya
kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita
inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu
Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
katika kuhakikisha tunakuwa na Utumishi wa Umma
3
wenye nidhamu, uwajibikaji wa hiari na utendaji wenye
matokeo kwa ustawi wa Taifa letu.
Ndugu Viongozi; Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma pamoja na majukumu mengine ya
kusimamia Uendelezaji Sera katika Utumishi wa
Umma, Utawala wa Utumishi wa Umma, Usimamizi wa
Rasilimaliwatu na Mishahara, Usimamizi wa Mifumo ya
TEHAMA ya Uendeshaji wa Serikali, Usimamizi wa
Mifumo ya Utendaji Kazi wa kila Siku Serikalini,
Uendelezaji Rasilimaliwatu, Usimamizi wa Serikali
Mtandao na Usimamizi wa Anuai za Jamii katika
Utumishi wa Umma, pia ina jukumu la KUSIMAMIA
MAADILI YA UTENDAJI KATIKA UTUMISHI WA
UMMA NCHINI.
4
Ndugu Viongozi; Mtakumbuka kuwa mnamo mwezi
Desemba 2022, tukiwa katika kilele cha maadhimisho
ya wiki ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa, moja
ya mambo muhimu tuliyoyafanya OR MUUUB ilikuwa
ni kutoa taarifa ya muhtasari wa matokeo ya “Utafiti
wa Hali ya Uzingatiaji wa Maadili katika Utumishi
wa Umma nchini kwa mwaka 2022” (Public Service
Integrity Survey 2022). Utafiti huu ambao ulifanyika
katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 uliongozwa na
Mtaalam Mwelekezi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe,
Kampasi ya Dar es Salaam kwa niaba ya OR MUUUB
ili kuweza kupata maoni huru. Utafiti huu umefanyika
kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo hojaji.
Ndugu Viongozi; Sote tunatambua kwamba Taasisi
za Umma ndio msingi mkubwa wa ufanisi katika
utekelezaji wa majukumu na mipango ya Serikali ya
kukuza uchumi, kutoa huduma bora kwa jamii na
kulinda amani na utulivu.
5
Taasisi hizo zimeundwa kwa ajili ya kufanikisha
jukumu la msingi la Serikali la kuleta ustawi kwa
Wananchi. Hivyo, ni wajibu wa Taasisi za Umma
nchini kuhakikisha zinafanikisha kufikiwa kwa malengo
ambayo Serikali imejiwekea Kitaifa na Kimataifa.
Malengo hayo ambayo Serikali imejiwekea
hayataweza kufikiwa endapo tutashindwa kuzingatia
na kusimamia vyema Maadili ya Utendaji katika
Utumishi wa Umma. Kwa kuzingatia hilo na dhamana
ambayo nimepewa na Serikali ya Awamu ya Sita
kusimamia masuala yote ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Ofisi yangu imekuwa ikitoa miongozo ya
Uzingatiaji wa Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa
Umma; kuwajengea uelewa wa masuala ya Maadili ya
Utendaji Watumishi wa Umma na Wananchi; na
kufanya Ufuatiliaji wa Uzingatiaji wa Miongozo hiyo.
6
Utafiti ni moja ya njia zinazotumiwa na Ofisi yangu
kutathmini Hali ya Uzingatiaji wa Maadili ya Utendaji ili
kuiwezesha Serikali kufahamu hali ya Maadili katika
Taasisi zake na kutumia mrejesho huo kutambua na
kufanyia kazi maeneo ambayo yana
kasoro/mapungufu ili kuimarisha utoaji wa huduma
kwa wananchi.
Ndugu Viongozi; Tathmini ya Hali ya Uzingatiaji
Maadili zinazofanyika katika Utumishi wa Umma
zinalenga kupata taarifa sahihi za usimamizi wa
Maadili ya Utendaji na Maadili ya Kitaaluma Katika
Utumishi wa Umma. Ili kuimarisha usimamizi wa
Maadili katika Utumishi wa Umma, katika mwaka wa
fedha 2021/2022 Ofisi hii iliendesha Utafiti wa Hali ya
Uzingatiaji wa Maadili katika Utumishi wa Umma wa
mwaka 2022 (Public Service Integrity Survey).
7
Lengo kuu ilikuwa ni kubaini endapo kumekuwa na
ongezeko la uzingatiaji wa viwango vya Maadili ya
Utendaji kwa Watumishi Umma.
Ndugu Viongozi; Kama ambavyo nilizungumza wakati
wa uzinduzi wa Tafiti hii, Tafiti ya kwanza ya Maadili
(Integrity Survey) katika Utumishi wa Umma ilifanyika
mwaka 2006 kwa lengo la kupata taarifa za msingi
kwa ajili ya kuweka kiwango cha uzingatiaji wa Maadili
(baseline information). Matokeo ya utafiti kwa mwaka
2005 yalionesha kuwa kiwango cha uzingatiaji wa
Maadili katika Utumishi wa Umma kilikuwa asilimia
56.4 (56.4%). Kiwango hiki ndicho kilichukuliwa na
kutumika kama “baseline” kwa kuwa awali hakukuwa
na utafiti wowote ambao uliwahi kufanyika kupima hali
ya uzingatiaji wa Maadili katika Utumishi wa Umma.
8
Mnamo mwaka 2014, ulifanyika utafiti mwingine ili
kufahamu endapo kumekuwa na ongezeko la
uzingatiaji wa viwango vya Maadili kwa Watumishi
Umma; na kubaini maeneo yenye mianya ya uvunjifu
wa Maadili kwa lengo la kuweka mikakati ya
uimarishaji inayoendana na matokeo halisi. Kwa
mwaka 2014 kiwango cha uzingatiaji wa Maadili
kiliongezeka toka 56.4% (ya mwaka 2005) hadi kufikia
asilimia 66.9 (66.9%).
Ndugu Viongozi; Utafiti wa mwaka huu wa 2022
umefanyika baada ya kipindi cha miaka minane (8)
kupita kutoka Tafiti ya mwisho iliyofanyika mwaka
2014. Lengo kuu la utafiti wa mwaka 2022 ilikuwa ni
kubaini kama kumekuwa na ongezeko la uzingatiaji
wa viwango vya maadili katika Utumishi wa Umma
(follow up study) ambapo Matokeo ya Utafiti wa Hali
ya Uzingatiaji wa Maadili katika Utumishi wa Umma
kwa mwaka 2022 yameonesha kuwa kiwango cha
9
uzingatiaji wa Maadili katika Utumishi wa Umma
kwa mwaka 2022 ni asilimia 75.9 (75.9%). Matokeo
haya yanaonesha kiwango cha uzingatiaji wa Maadili
katika Utumishi wa Umma kimeongezeka kwa wastani
wa asilimia 9.8 (9.8%) kwa mwaka 2022 ikilinganishwa
na 66.1% (ya mwaka 2014). Ongezeko hili la kiwango
cha Maadili linatokana na dhamira ya uongozi thabiti
wa Serikali Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu;
Programu za mabadiliko ya Kisekta na Taasisi
zenyewe; na utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa
Kupambana na Rushwa (NACSAP).
Ndugu Viongozi; Kwa mujibu wa matokeo ya taarifa
ya Utafiti huu, yapo maeneo ambayo bado yanahitaji
kuboreshwa / kutiliwa mkazo. Maeneo hayo ni pamoja
na:-
10
(i) Ufuatiliaji wa kila mara wa uzingatiaji wa kanuni za
maadili kwa watumishi wa umma;
(ii)Mafunzo endelevu kwa watumishi ambao wako
kazini; wale wanaoajiriwa kwa mara ya kwanza na
elimu kwa umma; na
(iii) Usimamizi wa uzingatiaji wa Maadili katika utoaji
wa huduma wakati wa majanga ya kitaifa kama vile
UVIKO-19 na majanga mengine mbalimbali
yanayotokea nchini.
Aidha, maeneo ambayo yameonekana kulalamikiwa
zaidi kutokana na kuwepo kwa viashiria vya kukithiri
kwa vitendo visivyo vya uadilifu ni pamoja na Jeshi la
Polisi; Mahakama; Manunuzi ya Umma, Mikataba; na
Huduma za Ardhi. Matokeo kuhusu maeneo ambayo
yamelalamikiwa zaidi kwa kiasi kikubwa
yanashabihiana na matokeo yaliyotolewa katika utafiti
wa kitaifa kuhusu Rushwa (National Governance and
11
Corruption Survey), utafiti ambao uliendeshwa na
TAKUKURU mwaka 2020, ambapo utafiti huo pia
ulibainisha kati ya Taasisi zinazolalamikiwa kuwa na
viashiria vya kujihusisha na vitendo vya rushwa ni
pamoja na Jeshi la Polisi; Mahakama; na Usimamizi
wa Ardhi.
Ndugu Viongozi; Tarehe 9 Desemba, 2022, wakati
wa uzinduzi wa matokeo ya utafiti huu kwa Umma
kupitia vyombo vya habari, nilitoa maelekezo katika
maeneo sita ya kufanyiwa kazi. Eneo la kwanza
ilikuwa ni kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kufanya kikao
kazi cha pamoja na wadau kwa ajili ya kufanya
majadiliano ya kina kuhusu matokeo ya utafiti huu na
kuja na mikakati ya ufuatiliaji wa uzingatiaji wa Maadili
katika sekta zote kulingana na matokeo.
12
Katibu Mkuu (UTUMISHI) ametekeleza maagizo haya
kwa kuandaaa mkutano huu kuhakikisha kuwa taarifa
ya Utafiti huu inawafikia. Hivyo niwaelekeze kupokea
taarifa hiyo ambayo itawasilishwa kwenu na Mtaalam
Mwelekezi; kuchambua kwa kina taarifa hiyo; na
kutoka na maazimio na mipango itakayowezesha
Serikali kuboresha Usimamizi wa Maadili ya Utendaji
katika Utumishi wa Umma.
Majadiliano yenu katika siku hizi mbili za kikao kazi
yazingatie mambo muhimu yafuatayo:-
(i) Kuweka mikakati ya kukuza Maadili inayoendana
na hali halisi;
(ii) Kubaini maeneo yenye changamoto za kimaadili
na kuishauri mamlaka ipasavyo;
(iii) kujitathmini kuhusu hali ya kimaadili ya
Watumishi wa Umma na kushauri hatua stahiki
13
kwa maeneo ambayo yameonekana kuwa na
mapungufu;
(iv) Kubaini maeneo ambayo yanafanya vizuri na
kuweka mikakati ya kuendelea kujiimarisha; na
(v) Kuendelea kuimarisha dhana ya ushirikishwaji
wa wananchi katika kuimarisha utendaji wa
Serikali kama moja ya misingi ya Utawala Bora.
Ndugu Viongozi; kwa kuwa kikao kazi hiki
kimeshirikisha Viongozi ambao wamepewa
dhamana ya kusimamia eneo la Maadili na Utawala
Bora katika Taasisi zao, nitumie fursa hii
kuwafahamisha maagizo mengine niliyoyatoa
tarehe 9 Desemba 2022 wakati wa uzinduzi wa
taarifa ya utafiti:-
(i) Taasisi Simamizi za Maadili na Utawala Bora
pamoja na Vyama vya Kitaaluma kuendelea
kushirikiana na OR - MUUUB kukuza Maadili na
14
kutumia matokeo haya kuimarisha mikakati ya
usimamizi katika maeneo yao;
(ii)Waajiri kuhakikisha wanatenga Bajeti ya mafunzo
ya Maadili na kuendesha mafunzo kwa watumishi
wa umma walio kazini na wale wanaoajiriwa. Kama
ambavyo mmesikia moja ya eneo ambalo
halikufanya vizuri ni eneo la mafunzo kwa
watumishi;
(iii)Waajiri kuhakikisha wanaweka na kuimarisha
mifumo ya utoaji wa mrejesho ndani ya Taasisi zao
ili kuendelea kutoa fursa kwa wananchi kukemea
vitendo vya ukiukwaji wa Maadili;
(iv)Waajiri kuendelea kutoa elimu kwa umma kupitia
njia mbalimbali ikiwemo Vyombo vya Habari na
Tovuti kuhusu haki na wajibu wa wananchi katika
kupata huduma bora katika Taasisi za Umma; na
15
(v) Viongozi na Watumishi wa Umma wote nchini
kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na
Taratibu zinazosimamia Utumishi wa Umma kwa
kuwa ndiyo nguzo kuu ya Maadili ya Utendaji katika
Utumishi wa Umma.
Ndugu Viongozi; Nichukue fursa hii tena
kuwapongeza watumishi wa umma pamoja na Taasisi
zote zilizofanya vizuri kwa mujibu wa utafiti huu, kwa
kuweza kuzingatia na kuyaishi maadili ya utendaji
katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Matarajio yangu ni kuwa washiriki wa mkutano huu,
mtafanya uchambuzi wa kina wa taarifa hii na kutoka
na maazimio ambayo yatasaidia kuimarisha hali ya
uadilifu katika Utumishi wa Umma na hatimaye kuwa
na Taasisi nyingi zaidi zinazofanya vizuri katika eneo
la Maadili.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇