Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, ameomba kufanya KIKAO MAALUM na Wakuu wa Sekondari zote 27 za Jimboni mwetu.
SEKONDARI 27:
*25 za Kata/Serikali
*2 za "private"
(KATOLIKI & SDA)
SIKU/TAREHE YA KIKAO:
*Ijumaa, 3.2.2023
MUDA:
*Saa 3 Asubuhi
MAHALI:
*Busambara Sekondari
Kijijini Kwikuba
AJENDA YA KIKAO:
*Mapendekezo ya UBORESHAJI wa KUJIFUNZA na KUFUNDISHA kwenye Sekondari zetu.
WAKUU WA SHULE waje na Matokeo ya Mitihani ya:
*Form II
(2022, 2021 & 2020)
*Form IV:
(2022, 2021 & 2020)
MATOKEO YA FORM IV (2022) YA SEKONDARI 5:
Matokeo ya Sekondari 5 za Jimboni mwetu yameambatanishwa hapa:
*Sekondari 3 za Kata:
(Etaro, Kiriba & Makojo)
*Sekondari 2 za "Private":
(Bwasi -- SDA & Nyegina - KATOLIKI)
SHULE ZA MSINGI:
Mbunge huyo atafanya KIKAO kama hicho na WALIMU WAKUU wa Shule zote za Msingi 118 za Jimboni mwetu. Tarehe itapagwa.
Mbunge huyo atagharamia:
*usafiri
*chakula
ELIMU NI NGUZO IMARA YA TAIFA
ELIMU NI UCHUMI
ELIMU NI MAENDELEO
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumatatu, 30.1.2023
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇