LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 7, 2023

LUDIGIJA ATAMBA HAKUNA MTOTO ATAKAYEKOSA KUSOMA DAR KWA UHABA WA MADARASA

Na Christopher Lissa

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija, amesema hakuna mtoto aliyechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza atakayekosa nafasi kutokana na kukosa darasa.


Shule  zinatarajiwa kufunguliwa keshokutwa nchini kote, Ludigija amewataka wazazi na walezi kuhakikisha kila mtoto aliyechaguliwa anaripoti shuleni. 


Alitoa mwito huo, alipokuwa akipokea madarasa 310 yaliyojengwa kwa Sh. Bilioni6.3 zilizotolewa na Rais Dk. Samia  Suluhu Hassan.


Katika hafla hiyo iliyofanyika Shule ya Sekondari Nguvu Kazi, Kata ya Chanika, Ludigija alisema, Rais Dk. Samia, alitoa fedha hizo kujenga madarasa 310 katika Halmashauri ya Jiji  la Dar es Salaam.


Alisema kwa mkoa mzima wa Dar es Salaam, Rais Dk. Samia alitoa kiasi cha sh. bilioni 12 kujenga madarasa.


“Ilala tulipata nusu ya fedha hizo yaani sh.  bilioni 6.2. Tumefanikiwa kujenga madarasa 273  ya msambao na yaliyosalia tuna jenga ghorofa,”alisema  Ludigija.

DC Ludigija (kushoto) akitoka kukagua madarasa wakati wa hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages