Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, Gerson Msigwa amesema kuwa kishindo kingine kikubwa cha uboreshaji sekta ya elimu nchini kinakuja. Amebainisha kuwa serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imetenga zaidi ya sh. trilioni moja kuboresha na kujenga miradi mingine katika sekta hiyo nchini. Amebainisha hayo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma Januari 15, 2023 kuhusu mafanikio ya miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Baadhi ya wanahabari wakiwa kazini
PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Gerson Msigwa akielezea kuhusu mradi huo mkubwa unaokuja katika sekta ya elimu....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDAMHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇