Afisa Elimu Wilaya ya Same, Amri Msemo amewaomba waumini wa dini zote kufanya Dua kwa ajili ya kupata mvua.
Amesema hayo kwenye sherehe ya Maulid iliyofanyika Same akiwa amemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Same, Edward Mpogolo, amewaomba watanzania kwa ujumla kufanya ibada kwa ajili ya kumuomba Mungu awezeshe kupata mvua itakayoleta faida kubwa kwenye kilimo na wananchi kupata mazao.
Aliendelea kusema hali ya mvua kutonyesha ni hali ya mabadiliko ya Tabia nchi kama watalaamu wetu wanavyosema kikubwa maombi yanahitajika kumuomba Mungu aweze kutujalia mvua.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇