Dar es Salaam, leo
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza kuyafuta matokeo ya mitihani ya Darasa la saba kwa shule za msingi zote zilizopo ndani ya Halmashauri ya Chemba, na baadhi ya shule katika Halmashauri ya Kondoa, Kinondoni, Mwanza jiji na Ubungo kwa kosa la kuhusika kwa kuvujisha kwa mitihani ya darasa la saba ikiwa ni kinyume na taratibu na kanuni za mitihani nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Taifa (NECTA) Charles Msonde amesema, “Kufuatia kuvunjwa kwa kanuni za mitihani baraza limeamua kufuta matokeo ya kumaliza shule ya msingi ya Halmashauri ya Chemba pamoja na shule ya Hazina na Kinondoni, Anyindumina na Font of Joy za Ubungo, Alloiance na New Alliance ya Mwanza jiji pamoja na Kondoa Integrity ya Kondoa Mjini, na watahiniwa wa mtihani hiyo watairudia tena oktoba tarehe 8 na tarehe 9 wiki ijayo." Amesema Charles Msonde.
Aidha baraza hilo limefuta vituo vya mitihani kwa shule nane ambazo zilihusika katika uvujishaji wa mitihani hiyo sambamba na kupendekeza kuondolewa kwenye nafasi za ajira kwa baadhi ya maafisa elimu kata na wilaya waliohusika kwenye udanganyifu huo.
Your Ad Spot
Dec 1, 2022
Home
featured
Kitaifa
NECTA YAFUTA MATOKEO YOTE YA LA SABA HALMASHAURI YA CHEMBA NA BAADHI YA SHULE KINONDONI, KONDOA, UBUNGO NA MWANZA JIJI
NECTA YAFUTA MATOKEO YOTE YA LA SABA HALMASHAURI YA CHEMBA NA BAADHI YA SHULE KINONDONI, KONDOA, UBUNGO NA MWANZA JIJI
Tags
featured#
Kitaifa#
Share This
About CCM Blog
Kitaifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇