Na Bashir Nkoromo, CCM Blog.
Jumapili ya Disemba 4, 2022 ilikuwa siku ya heka heka ya aina yake wakati vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Saranga, Ubungo Jijini Dar es Salaam, walipofanya kazi nzuri ya kijamii kwa kupanda na kushuka milima na mabonde katika Kata hiyo na kuwafikia wenye mahitaji maalum kisha kuwapa misaada ya vitu mbalimbali.
Licha ya Kata hiyo ya Saranga kuwa na milima na mabonde kila eneo, huku jua likiwa kali na vumbi likitimka Vijana hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Kata hiyo Rachel Masaki na Katibu wake Benson Mhina siku hiyo waliweza kuzifikia Kaya saba (7) za wenye mahitaji maalum na kuzigawia vitu hivyo.
Baadhi ya waliofikiwa na vijana hao ni Mama mmoja mkazi wa mtaa wa Mnarani Sakina Sadiki ambaye anaishi na mtoto Munira Abdallah mwenye umri wa miaka 14, ambaye anachangamoto ya maradhi ya kichwa kuwa kikubwa kupita kiasi na shida ya macho kutoona vizuri.
Mwingine ni Bibi Ameria Stanslaus anayefahamika zaidi kwa jina la Bibi wa Kihaya ambaye licha ya yeye mwenyewe kuwa mzee lakini anaishi na kuwatunza watoto wawili, mmoja mwenye ugonjwa wa afya ya akili na mwingine wa kiume anayeugua kifafa.
Pia vijana hao walifika kwenye familia ya Elizabeth Mkwela ambaye anaishi na mtoto mwenye ugonjwa wa kupooza mwenye umri wa miaka minne na Mama mwingine anayeishi na familia ya watoto wanne katika makazi duni na hana shughuli maalum.
Vijana hao walimalizia mchakamchaka huo kwa kufika nyumbani kwa Winingiael Abdulrahman ambaye anafanya kazi ya ulinzi huku akilea mtoto wake mwenye ulemavu wa kupooza ambapo ili aweze kwenda kazini usiku kufanya kazi hiyo ya ulinzi hulazimika kumuacha mtoto huyo mwenye ulemavu wa kupooza aliangaliwa na dada yake ambaye bado ni mwanafunzi wa darasa la saba.
Baadhi ya vitu ambavyo vijana hao wa UVCCM walivigawa kwenye Kaya hizo zenye mahitaji ni pamoja na Mchele, sukari, maharage, mafuta ya kupikia, viti maalum vya watoto wenye ulemavu na miche ya sabuni za kufulia.
"Mimi pamoja na vijana wenzangu hawa pamoja na marafiki zangu kwa pamoja tumejitahidi kupata hiki kidogo tulichojaliwa, basi tunakuomba upokee, ", alisema Rachel kwa nyakati tofauti kila vijana hao wa UVCCM walipokuwa wakifika na kukabidhi msaada huo.
"Mnajua hawa wote tuliowafikia kuwapa misaada hii, kama tunavyoona changamoto kubwa waliyo nayo ni uchumi, sasa awamu nyingine tutatafuta namna ya kuziwezesha hizi kaya zenye mahitaji maalum, ili ziweze kujishughulisha na shughuli za kujitafutia kipato ili walau wakijimu", akasema Rachel.
Rachel akawaomba wote watakaojaliwa kupata uwezo wawe wanatembelea kaya hizo kila mmoja kwa muda wake na kusaidia kupunguza chanagamoto zilizopo.
Pia Rachel alisema, ameshafanya jitihada za kuzipatia Bima ya Afya Kaya hizo zenye mahitaji maalum, lakini imekuwa ikishindikana kwa kuwa kaya hizo hazina nyaraka za utambulisho kama za kuzaliwa ambazo hutolewa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (Registration Insolvency and Trusteeship Agency - RITA).
"Nilitamani sana watu hawa tuwapatia Bima za Afya, lakini jitihada zangu zimekwama kwa sababu, hizi kaya zenye mahitaji maalum hawana hati za kisheria hasa vyeti vya kuzaliwa amvavyo hutolewa na RITA."akasema Rachel.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Saranga Rachel Masaki akiwa na Vijana wenzake wa UVCCM wakati akimkabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Bibi Ameria Stanslaus anayefahamika zaidi kwa jina la Bibi wa Kihaya ambaye licha ya yeye mwenyewe kuwa mzee lakini anaishi na kuwatunza watoto wawili, mmoja mwenye ugonjwa wa afya ya akili na mwingine wa kiume anayeugua kifafa.
Sasa endelea kuona matukio katika picha hapo👇
Viana wa UVCCM Kata ya Saranga wakiwa katika maandalizi ya kuanza safari ya kwenda katika maeneo mbalimbali ya Kata hiyo kutoa misaada kwa Kaya zenye mahitaji maalum |
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Saranga Rachel Masaki akiandaa katika gari vitu mbalimbali ili kuanza kuvigawa kwa wenye mahitaji
Vijana wa UVCCM Saranga wakibeba vitu mbaimbali wakati msafara ukienda kukabidhi kwenye kaya moja ya mwenye mahitaji.
Mwananchi wa Kata ya Saranga akitoa mwanae baada ya Vijana hao wa UVCCM kufika nyumbani kwake kutoa msaada huo. Mwanae huyo ana tatizo la kichwa kuwa kikubwa kuliko kawaida na shida ya kutoona.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Saranga Rachel Masaki akizungumza kwa niaba ya wenzake nyumnai kwa Mama huyo kabla ya kukabidhi msaada.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Saranga Rachel Masaki akiendelea kuzungumza.
Mama akiwa na mwanae mwenye matatizo ya kichwa kuwa kikubwa kuliko kawaida,
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Saranga Rachel Masaki na Vijana wenzake wakimpatia mama huyo msaada wa vitu mbalimbali.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Saranga Rachel Masaki na Vijana wenzake wakiendelea kumgawia mama huyo msaada wa vitu mbalimbali.
Kisha Rachel na wenzake wakaendelea na safari ya kupanda vilima na mabonde kwenda kwingine baada ya kutoka kwa mama huyo.👇
'Mama wa Kihaya' akiwakaribisha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Saranga Rachel Masaki baada ya yeye na Vijana wenzake wa UVCCM kufika nyumbani kwake kutoa msaada wa vitu mbalimbali.
Katibu wa UVCCM Kata ya Saranga Benson Mhina akifanya utambulisho baada ya kufika nyumbani kwa 'Mama wa Kihaya' huyo kugawa msaada.
"Namshukuru Mungu, na Ninyi nawashukuru sana kuja kunipa msaada huu, asanteni sana, sana, sana na Mungu awabariki", 'Mama wa Kihaya' akasema kumwambia Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Saranga Rachel Masaki ambaye alionekana kumsikiliza kwa makini.
Kisha Mwenyekiti huyo wa UVCCM Kata ya Saranga Rachel Masaki akamkabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa 'Mama wa Kihaya huyowa na Vijana wenzake wa UVCCM wakatim
'Mama wa Kihaya' huyo akifurahia mche wa sabuni ya kufulia ambao ni miongozi wa vitu mbalimbali alivyokabidhiwa na vijana hao wa UVCCM.
Jirani akizungumza jambo na Mama huyo.
Jirani huyo akaendelea kuzngumza ikiwemo kumpongeza Mama huyo kwa kupata msaada wa Vijana hao.
Kisha safari kwenda kwingine ikaendelea tena👇
Wakamkabidhi vitu mbalimbali na kiti maalum cha kumuwezesha mtoto huyo kukaa.
Mwenyekiti wa Umoja wa UVCCM Kata ya Saranga Rachel Masaki akiwa na Vijana wenzake wa UVCCM wakati akimkalisha vema mtoto huyo.
Kisha wakapata picha ya kumbukumbu na mtoto huyo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Saranga Rachel Masaki akiwa na badhi ya Vijana wenzake wa UVCCM pamoja na mtoto huyo.
Kisha safari ya kwenda kwingine ikaanza tena👇
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Saranga Rachel Masaki akizungumza nyumbani kwa bibi huyo huku akiwa na wenzake.
Rachel akiendelea kuzungumza
Kisha Rachel akakabidhi fedha kiasi kwa ajili ya kumsaidia Bibi huyo kumlea mtoto huyo mwenye shida ya tumbo.Wakapiga picha ya kumbukumbu
Halafu wakamuaga. Safari ya kwenda kwingine ikaendelea👇
Kisha picha ya pamoja
Wafurahi kutoa msaada Kisha wakaenda kwingine👇
Makazi ya mmoja wa wenye mahitaji ambaye hata hivyo wakati vijana hao wanafika hakuwepo ikabidi msada wakabidhiwe majirani mbele ya Katibu wa CCM wa Tawi
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Saranga Rachel Masaki akizungumza kabla ya kukabidhi msaada na wenzake
Kisha Rachel akakabidhi msaada kwa jirani wa mwenye mahitaji ambaye hakukutwa kwenye makazi yake.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇