LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 28, 2022

KIKUKWE DAY KAGERA YAFANA, VIPAUMBELE KUELEKEA 2023 VYAMKUNA MBUNGE WA NKENGE

Mbunge wa jimbo la Nkenge Florent Kyombo akiendesha harambee ya kuchangia maendeleo.

Sehemu ya watoto walioonyesha vipaji vyao



Mbunge wa jimbo la Nkenge Florent Kyombo akitoa vyeti vya shukrani kwa wazee waliojituma na kuleta maendeleo kijijini Kikukwe.

Katibu wa umoja wa maendeleo Kikukwe (UMKI) Bi Magreth Kyai akizungumzia vipaumbele vya utekelezaji kuelekea mwaka 2023.

Mwenyekiti wa umoja wa maendeleo (UMKI) Godfrey Mugini akizungumza katika sherehe hizo.


Na Lydia Lugakila, Kagera.


Sherehe za umoja wa maendeleo Kikukwe  (UMKI) zimefana huku vipaumbele kwa utekelezaji kwa mwaka 2023 vikimkuna mbunge wa jimbo la Nkenge wilayani Misenyi na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wananchi kwa asilimia 100.


Umoja wa huo wenye lengo la kusukuma maendeleo mbele na kuiunga mkono serikali umefanyika ikiwa ni mara ya pili katika kata ya Kanyigo wilayani Misenyi mkoani Kagera ambapo mbunge wa Jimbo la Nkenge Florent Kyombo ameeleza namna atakavyowaunga mkono wananchi kupitia bajeti kuu ya serikali.


Hatua hiyo imekuja baada ya Kutibu wa umoja huo Bi Magreth Kyai kubainisha vipaumbele vya utekelezaji kwa mwaka 2023 vilivyojipambanua katika kuongeza maendeleo katika kata hiyo.


Bi Kyai amesema kuwa katika upande wa Elimu umoja huo utahakikisha Bweni la wasichana Kikukwe sekondari linajengwa na kukamilika mwaka 2023, ili kuondoa changamoto ya wanafunzi kutumia vyumba vya madarasa kama bweni, kutafuta walimu wa kufundisha masomo ya ziada kwa shule za msingi na sekondari ili kuongeza ufaulu, kufuatilia mpango wa kuanzisha kidato cha tano na sita kwa shule ya sekondari Omurushenye, kubuni vitega uchumi ili kujiendeleza kibiashara, watoto waliofaulu kuhakikisha hawabaki majumbani.


Mbunge huyo aliyemwakilisha mkuu wa wilaya ya Misenyi ameupongeza umoja huo katika kusukuma maendeleo katani humo na kuwa kutokana na ukubwa wa mradi huo ikiwezekana atawaunga mkono kupitia bajeti kuu ya serikali ili kuwawezesha kusukuma maendeleo.


"Kwa hamasa hii mimi sijawahi ona niwapongeze kwa namna mnavyoisaidia serikali ki maendeleo naahidi shilingi laki 5, na kutoka katika mfuko wa mbunge utachangia shilingi  milioni 5 na ahadi ya mkuu wa wilaya ya Misenyi ni shilingi laki 3 hongera sana kwa namna mnavyochangia maendeleo"alisema Kyombo.


Akitoa salamu za Rais Dkt Samia mbunge huyu amesema kuwa serikalini haitawaacha nyuma kwani katika kufanya mradi wa kupeleka umeme kwenye vitongoji wapo hatua za mwisho huku akikitaja kitongoji cha kwanza kupata umeme kuwa kitakuwa Nyungwe ambapo amewaomba wananchi hao kuzidi kumwamini Rais Dkt Samia.


Aidha Katibu wa umoja huo Bi Kyai amesema kuwa wameweza kufanya pia mikakati ya kuwaodoa wanyama waharibifu wa mazao kama ngedere, kuwa na bima ya maisha na ujenzi.


Aidha amewahimiza wana UMKI waishio nje ya kata hiyo wakiwemo wa mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Mwanza Morogoro Arusha na Bukoba kuendelea kudumisha umoja huo huku akihidi kuwa wamejipanga kuhamasisha kila kitongoji kusafisha barabara za ndani ya kijiji   hicho.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja wa maendeleo -UMKI Godfrey Mugini amesema kuwa watahakikisha pia umoja huo unaunga mkono juhudi za serikali katika kusukuma maendeleo huku akitoa vyeti vya shukrani kwa wazee ambao wamekuwa mstari wa mbele kujituma na kujitoa katika kuleta maendeleo kijijini humo akiwemo mzee Iddi Khalfan Kakoka, Lichard Lweyemamu na Maico Nkumba.


Hata hivyo katika sherehe hizo wananchi na viongozi wamechangia maendeleo ya kijiji Kikukwe huku mbunge wa jimbo la Nkenge akiweka jiwe la msingi ujenzi wa bweni la wasichana shule ya sekondari Kikukwe.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages