LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 12, 2022

SHAKA: WATANZANIA TUTAMPA RAIS SAMIA TUZO YA HESHIMA 2025

Kigamboni, Dar es Salaam
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema kutokana na kazi nzuri anayofanya Rais Samia Suluhu Hassan, Watanzania watampa tuzo iliyotukuka na ya heshima mwaka 2025.

Amesema Rais Samia meonyesha uungwana wa hali ya juu kwa kuendelea kuchapa kazi yenye tija na kuleta matokeo mazuri ikiwemo kutekeleza miradi ya maji yenye lengo la kupunguza na kuondoa changamoto ya upatikanaji wake katika maeneo mbalimbali nchini.

Shaka ameyasema hayo leo Novemba 11, 2022 wakati akizindua mradi maji wa Kimbiji uliopo Kigamboni Dar es Salaam na kukabidhi mitambo ya kutafuta na kuchimba visima virefu vya maji na kukabidhi eneo la uchimbaji bwwa la Kidunda kwa mkandarasi atakayetekeleza mradi huo.

"Kwa heshima unayoileta Watanzania watakupa tuzo iliyotukuka na ya heshima mwaka 2025.

"Mheshimiwa Rais Samia hongera sana kwa mzigo huu unaochapa yuko mshairi alisema na yuko mshairi alitunga tungo 'ada ya mja ni kunena' akimaanisha kwamba kawaida ya binadamu ni kusema 'muungwana ni vitendo na kila aliyemuungwana atatenda. Mheshimiwa Rais wewe ni muungwana wa taifa hongera sana.

"Akamalizia (mshairi) kusema tenda watu wataona majigambo weka kando. Mheshimiwa Rais unatenda, huna zogo, huna mbwembwe unawaletea maendeleo wananchi vijana wa mjini wanasema unakimbiza kimyakimya," amesema.

Amesema pamoja na ukame uliopo kwa sasa ambao umesababisha upungufu wa maji katika maeneo mbalimbali serikali inafanya kazi nzuri na kwamba Chama kuanzia kamati za siasa za wilaya, mikoa, sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa na wajumbe wa Halmashauri Kuu, wametembelea na kujiridhisha kuna miradi ya maji 1,194, hivyo nchi nzima inaguswa na utekelezaji huo. Msikie Shaka akiunguruma Hapo👇


 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages