LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 3, 2022

RC SINGIDA AFANYA ZIARA IKUNGI KUFUATILIA MGOGORO WA VIONGOZI

Mkuu wa mkoa wa Singida Peter Joseph Serukamba amefanya ziara wilayani Ikungi katika kijiji cha Choda kata ya Mkiwa na kuzungumza na viongozi wa Halmashauri ya kijiji pamoja na kusalimiana na wananchi wa kijiji cha choda 


RC Serukamba amelazimika kuzungumza na viongozi wa Halmashauri ya kijiji cha Choda katika kuhakikisha anaumaliza mgogoro wa viongozi wa kijiji hicho mara baada ya baadhi ya wananchi na viongozi kumuomba aingilie kati utata wa mgogoro huo


Akizungumza na viongozi hao Rc Serukamba amesema kwa mujibu wa maelezo aliyoyapata kutoka kwa viongozi wa halmashauri ya kijiji, pamoja na viongozi wa CCM wa tawi na kata amebaini tuhuma zinazotolewa dhidi ya Mwenyekiti wa kijiji hicho hazina mashiko ya kumuondoa katika nafasi yake 


Awali Mkuu wa wilaya ya Ikungi Jerry Muro akitoa taarifa ya jinsi walivyoshughulikia mgogoro huo amesema walilazimika kufanya vikao vitatu vya kutatua changamoto hiyo ambapo katika kikao cha mwisho mwezi Oktoba 2022  Muro aliwataka kufuata utaratibu endapo wanaona tuhuma za kumtoa Mwenyekiti wa kijiji zina ukweli jambo ambalo baadhi ya viongozi hawakufanya hivyo. 


RC Serukamba mbali na kupongeza jitihada za awali za wilaya katika kutatua mgogoro huo amewataka wajumbe wa halmashauri ya kijiji na viongozi wa ccm tawi kufanya kazi na mwenyekiti huo na kumpa ushirikiano ili atekeleze majukumu yake ipasavyo na kuwaonya baadhi ya wajumbe kuacha kuweka maslahi yao binafsi.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages