LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 9, 2022

RAIS SAMIA AMPONGEZA BALOZI WA MAZINGIRA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU CCM KIGAMBONI WINFRIDA SHONDE

Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi na Mshauri Elekezi wa masuala ya mazingira (Environmental Consultant) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kigamboni, Dar es Salaam, Winfrida Shonde, alipotembelea Banda la Maonyesho la Tanzania ndani ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Sharm El Sheikh, nchini Misri, jana, Novemba 8, 2022.

Wakisalimiana,  Rais Samia alimpongeza Winfrida kwa kuwa msichana ambaye anafanya vizuri katika masuala ya mazingira Tanzania.

Naye Shonde alimweleza Rais kwamba ataendelea kusaidia juhudi za Serekali katika upande wa Mazingira na kusapoti juhudi za mheshimiwa Rais  Samia ambazo anazifanya kila siku kuhakikisha Tanzania inapiga hatua katika nyanja zote ikiwemo uchumi na Diplomasia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mabalozi wa Mazingira wa Tanzania Winfrida Shonde, baada ya kutembelea Banda la Maonesho la Tanzania lililopo ndani ya ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Sharm El Sheikh, nchini Misri jana, Novemba 8, 2022.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages