LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 10, 2022

 RAIS SAMIA AIPONGEZA YANGA KWA KUTINGA HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameipongeza timu ya Yanga (Young African Sports Club) kwa kufanikiwa kuingia hatua ya makundi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

"Kongole Yanga SC kwa ushindi na kufanikiwa kusonga mbele katika michuano ya soka la Wanaume kwenye Kombe la Shirkisho Afrika, msimu wa 2022/2023. Nawatakia kila la kheri katika hatua inayofuata", ameandika leo pongezi hizo Rais Samia, katika kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Yanga ambao ndiyo mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara jana Noveamba 9, 2022 walifuzu kuingia hatua hiyo ya makubdi katika Michuano ya Kombe la  hilo la Shirikisho baada ya kuidungua bao 1-0 wenyeji wao Club Africain katika mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Le Stade Olympique de Rades Jijini Tunis, Tunisia.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages