LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 29, 2022

RAIS DK. MWINYI AFUNGUKA KATIKA KONGAMANO MJINI RIYADH

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inategemea pato la nchi kwa asilimia 29.2% katika sekta ya Utalii huku akieleza kuwa Serikali imeweka hatua za makusudi  katika mazingira wezeshi kwa kujumuisha sera, mifumo ya kitaasisi na kisheria ili sekta hiyo ikue kwa njia endelevu.

 Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo katika Kongamano la Kimataifa la 22 la WORLD 🌎 Travel &Tourism  Council Global Summit lililofanyika  jijini Riyadh,Saudi Arabia katika Hoteli ya Ritz-Carlton ambapo amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan. 

Aidha, alisema ukuaji wa sekta ya Utalii  inatarajiwa kuwavutia wageni wenye uwezo mkubwa ambao watatumia fedha zaidi ili kulinda rasilimali za bahari pamoja na uchafuzi wa Mazingira. 
Akifungua Kongamano hilo Waziri wa Utalii wa Saudia Arabia Mhe.Ahmed Al Khateeb amesema anatarajia majadiliano ya Kongamano  hilo yatoe njia sahihi za kutatua changamoto za Utalii,Usafirishaji na Mazingira kwa ujumla.

Pia,Kongamano hilo limehudhuriwa na Viongozi  kutoka Mataifa mbalimbali Duniani ambapo walipata fursa ya Kuchangia .

 Kongamano hilo la 22 la  WORLD 🌎 Travel  &Tourism  Council Global Summit limeongozwa na Mwandishi nguli nchini Marekani wa CBS ,Peter Greenberg ambaye alikuwa mtayarishaji wa filamu ya Royal Tour Tanzania 


📆 28 November 2022
đź“ŤRitz-Carlton, Riyadh Saudi Arabia

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages