Makundi ya kutetea haki za binaadamu na jamaa za wanaharakati wa kishia, waliohukumiwa kifo, wamemtolea mwito Papa Francis kutumia ziara hiyo kuitaka serikali kufuta hukumu ya kifo na ukandamizaji wa kisiasa Bahrain.
Ziara hii ya siku nne ni ya kwanza ya kiongozi huyo wa waumini wa kikatolili bilioni 1.3 duniani kuifanya Bahrain, anakotarajiwa kushiriki mkutano wa dini unaohimiza utangamano kati ya nchi za Mashariki na za Magharibi.
Kiongozi wa masuala ya misikiti mjini Manama Sheikh Habib al Namliti amesema watakutana na Papa kwa lengo moja la kuhakikisha dunia inafikia kwa pamoja amani na usalama wa chakula.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇