, Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Festo Ndugange akiwa na Mbunge wa Same Mashariki Mhe Anne kilango akikagua majengo ya kituo cha Afya kata ya Vunta na kutoridhishwa na hadhi ya kituo hicho.
Dkt. Ndugange amesema serikali imetoa milioni mia tatu za awali kujenga kituo kipya cha Afya vunta ambacho kitajegwa na jengo la upasuaji na chumba cha kuhifadhia maiti.
Ameendelea kusema Pesa hizo zimetolewa na Raisi Samiha Suluhu Hassani kuhakikisha wananchi wa kata ya vunta wanapata Huduma bora ya Afya
Wakati akiwa kwenye ziara hiyo amemshukuru Mhe Anne kilango kwa juhudi kubwa anazofanya kuwapambania wananchi wa jimbo lake akiwa bungeni.
Pia nakusema amevutiwa na miradi mikubwa ya jimbo hilo ikiendelea vizuri ujenzi wa Madasa ya Shule ya Sekondary ya Mihamba na zahati kubwa ya kisasa ambayo imegharimu milioni mia tano za ujenzi wake ikikaribia kukamilika hivi karibu.
Pia amesema serikali itashirikiana na Tarura kuhakikisha barabara zote ambazo zinajegwa hili kuleta unafuu kwa wakazi wa vijiji vya Same Mashariki kakamilika kwa wakati
Naibu waziri Festo amewaomba wananchi wa jimbo la Same Mashariki kumuunga mkono Raisi Samiha Suluhu Hassani kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo kwa wananchi wake
Mhe Anne kilango amesema anatoa shukran sana kwa Raisi Samiha Suluhu Hassani kwa kumpatia milion mia tatu kwa ajiri ya ujenzi wa kituo cha Afya vunta ambacho alikisemea akiwa bungeni zaidi ya mara tatu na leo utejelezajiwake unakwenda kukamilia.
Pia ameendelea kusema lengo lake ni kuona wananchi wake hawapati tabu kwenye mahitaji muhimu kama Afya,Elimu, Maji, na barabara hili waweze kupitisha mazao yao kwa wepesi zaidi na ataendelea kuwapatia wananchi wake miradi tofauti wajikwamue kiuchumi
picha na Ashrack Miraji
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇