Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Mujungu Masyenene akielezea lengo la kuanzisha Kituo Jumuishi katika Soko jipya la Machinga jijini Dodoma, ambapo wamachinga wa soko hilo watakuwa wanapata huduma eneo moja na kwa wakati kupitia taasisi mbalimbali za serikali na watu binafsi.Kulia ni Afisa Urasimishaji na Uendelezaji Biashara wa MKURABITA, Zabron Makoye
Masyenene ameelezea hilo baada ya kufanya kikao na wawakilishi wa taasisi mbalimbali kilichofanyika jijini Dodoma Novemba 2, 2022.
Pia MKURABITA na taasisi hizo zimeamua kutoa mafunzo kwa wamachinga ili kuwapa uelewa wa uendeshaji wa biashara zao pamoja na kunufaika na mikopo kutoka taasisi za fedha.
Afisa Urasimishaji na Uendelezaji Biashara wa MKURABITA, Zabron Makoye akielezea jinsi MKURABITA itakavyoweka utaratibu wa mafunzo kwa wamachinga.
Afisa Utafiti na Ufuatiliaji wa MKURABITA, Francis Mujuni akielezea kuhusu dodoso ya kukusanya taarifa za wamachinga na kutengeza kanzi data.
Baadhi ya washiriki kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika kikao hicho.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video,Masyenene akielezea mpango wao huo....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDAMHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇