LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 18, 2022

MWENYEKITI UWT WILAYA YA KIGAMBONI MWAJABU MBWAMBO APANDA CHEO KWA KISHINDO NA KUWA MWENYEKITI WA UWT MKOA WA DAR ES SALAAM

Na Bashir Nkoromo, Sinza
Mwajabu Mbwambo ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Kigamboni, amepanda cheo na kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoa wa Dar es Salaam, baada ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT mkoa huo kumchagua kwa kishindo, jana.

Katika Uchaguzi huo uliofanyika Sinza jijini Dar es Salaam, Mwajabu alijinyakulia jumla ya kura 164 kati ya kura halali 271 zilizopigwa na wajumbe, wote 303 wa Mkutano huo Mkuu na hakuna kura iliyoharibika.

Akitangaza matokeo, Msimamizi wa Uchaguzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'walabuzu Ludigija  alisema wengine watatu waliokuwa katika kinyang'anyiro na Mwajabu, kura walizopata zikiwa katika mabano, ni Marie Kigalu (104), Angel Myai (2) na  Saraha Osima (moja).

Nafasi nyingine ya juu iliyopambaniwa katika uchaguzi huo ni Ujumbe wa Baraza Kuu la UWT mkoa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM ambapo  Doreen Alfred Kahwa, aliibuka kidedea kwa kujikusanyia kura 187 na akiwashinda wagombea wenzake watatu, Nuru Awadhi Angelina Akilimali na Emiliana James.

Zingine zilikuwa ni Uwakilishi kutoka UWT mkoa kwenda kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM mkoa, UWT kwenda Mkutano Mkuu wa Wazazi mkoa na UWT kwenda Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoa  na Ujumbe wa Baraza Kuu UWT mkoa.

Akizungumza kabla ya kuachia kiti, Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, aliyemaliza muda wake Florence Masunga aliwataka Wanachama na Viongozi wote wa UWT mkoa huo kumuunga mkono kwa dhati Mwenyekiti wao mpya Mwajuma.

Masunga alieleza furaha yake kwamba ameiacha UWT mkoa huo ikiwa katika mikono salama huku akijivunia kwamba aliyoacha si haba, kwa kusema kwamba akishirikiana na wanachama na Viongozi wenzake wa UWT akiwemo Katibu wa Jumuiya hiyo mkoa Paulina Bupamba katika kipindi kifupi wameweza kutekeleza miradi mbalimbali kwa mafanikio ikiwemo ujenzi wa nyumba za Makatibu wa UWT Wilaya.

Mkutano huo Mkuu ambao Kamisaa wa Uchaguzi alikuwa Bupamba, ulihudhuriwa pia na Mwenyenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Mama Kate Slyvia Kamba amabaye sasa amejitupa katika kinyang'anyiro cha kuwania Uenyekiti wa UWT Taifa, na pia alihudhuria Katibu wa CCM mkoa huo Adamu Ngalawa ambaye pia alikuwa katika jopo la kusimamia uchaguzi.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga akimpongeza Mwenyekiti mpya wa UWT mkoa huo Mwajabu Mbwambo baada ya matokeo ya Uchaguzi uliofanyika Sinza jijini Dar es Salaam, jana.
Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Paulina Bupamba akizungumza na kufanya utambulisho wa viongozi mbalimbali mwanzoni mwa mkutano huo.
Viongozi meza kuu wakifanya sala kabla ya kikao kuanza, sala hiyo iliongozwa na Katibu Bupamba.
Wajumbe ukumbini
Wajumbe ukumbini.Wajumbe ukumbini.
Wajumbe ukumbini.
Wajumbe Ukumbini.
Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Paulina Bupamba akiendelea na utambulisho..
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Mama Kate Slvia Kamba akizungumza kusalimia Wajumbe kwenye mkutano huo.
Msimamizi wa Uchaguzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'walabuzu Ludigija akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga akitangaza kujiuzulu yeye na safu yake ya uongozi kupisha Uchaguzi wakati wa mkutano huo.
Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Adamu Ngalawa ambaye alikuwa katika jopo la wasimamizi wa Uchaguzi katika mkutano huo, akizungumza.
Mgombea Nuru Awadhi Abdallah mwenye ulemavu wa kuona akiomba kura nafasi ya Ujumbe wa Baraza Kuu la UWT mkoa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM.
Anjelina Akilimali akiomba Ujumbe wa Baraza Kuu la UWT mkoa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM
Doreen akiomba Ujumbe wa Baraza Kuu la UWT mkoa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM
Wagombea Uwakilishi wakipewa utaratibu.
Baadhi ya Wajumbe wakila chakula cha mchana wakati yakisubiriwa matokeo ya uchaguzi.
Kamishna wa Uchaguzi huo, Katibu wa UWT mkoa wa dar es Salaam Paulina Bupamba na Msimamizi wa Uchaguzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'walabuzu Ludigija wakiweka mambo sawa muda mfupi kabla ya kutangaza matokeo.
Wajumbe wakijimwaya mwaya ukumbini kupongeza baada ya kupata 'matokeo' ya awali.
Katibu Bupamba akimkaribisha Msimamizi wa Uchaguzi kutangaza matokeo.
Msimamizi wa Uchaguzi Ludigija akitangaza matokeo. Kushoto ni Katibu Pubamba na Mwenyekiti wa Kikao cha Uchaguzi, Mwenyekiti wa UWT Mstaafu Florence wakifuatilia matokeo hayo.
Viongozi waliochaguliwa katika nafasi mbalimbali wakiwa wamejipanga mbele ya meza kuu wakati Msimamizi wa Uchaguzi akitangaza matokeo ya Nafasi ya Mweneyekiti wa UWT mkoa.
Mwenyekiti mpya wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Folrence Masunga akitoa hotuba ya mwisho kuelezea yaliyofanywa na uongozi wake. Mwenyekiti mstaafu Masunga akimpongeza Mwenyekiti mpya Mwajabu Mbwambo.
Mwajuma Mbwambo akisalimia wajumbe baada ya kukaribishwa meza kuu.mm

Mwenyekiti mpya wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo akihutubia baada ya kukalia rasmi kiti chake cha Uenyekiti meza kuu.
Wajumbe wakimsangilia
Wajumbe wakijimwayamwaya mbele ya Mwenyekiti wao mpya.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam Janeth Mahawanga na Mbunge wa Viti Maalum Vyuo Vikuu Dk. Paulina Nahato (kushoto) wakishangilia wakati Mwenyekiti Mpya Mwajabu akizungumza, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam Janeth Mahawanga na Mbunge wa Viti Maalum Vyuo Vikuu Dk. Paulina Nahato (kushoto) wakiwa wameketi huku wakiendelea kufuatilia kwa furaha hali ya mambo ukumbini.
Mwenyekiti mpya Mwajabu na Katibu Bupamba wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wapya waliochaguliwa.
Mwenyekiti mpya Mwajabu na Katibu Bupamba wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wapya waliochaguliwa.
Makatibu wa UWT Wilaya za Dar es Salaam, wakiwa na viongozi mbali wakiwemo wapya waliochaguliwa

©Nov. 2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages