Mkuu wa wilaya ya Same, Edward Mpogolo ameshiriki kikamilifu kwenye Fainali ya Anne Kilango Cup.
Akiwa Mgeni Rasmi Dc Mpogolo alimpongeza mbunge wa Same Mashariki, Mhe Anne Kilango kwa kuanzisha mashindano ya mpira wa miguu na kusema kwamba mashindano haya yanaleta umoja na mshikamo kwa vijana na kukuza vipaji vyao.
DC Mpogolo aliendelea kusema lengo la mashindano kutoa Elimu juu ya Utunzaji wa Mazingira na kuhamasishana vijana wenyewe kufanya kazi hili kujenga nchi yetu hasa kwenye kilimo
Pia Mbunge wa Same Mashariki Mhe Anne Kilango amesema mashindano haya ni endelevu na lengo ni kuwaweka vijana wawe pamoja na kutengeneza timu ya jimbo ambayo itakayofanya vyema kwenye mashindano makubwa
Pia ameendelea kusema zaidi ya vijana 1200 wameshiriki mashindano haya na kusisitiza kuwa mashindano haya ni juhudi za kumuunga mkono Raisi Samiha Suhuru Hassani kwani na yeye ni mmoja wa wadau wanaopenda michezo hapa nchini
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇