Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha sarakasi Tanzania (CHASATA) kimeandaa uzinduzi wa kuinua vipaji vya mchezo huo utakaofanyika Jumamosi jioni kwenye ukumbi wa makumbusho ya Taifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa chama cha sarakasi Tanzania, Selemani Pembe alisema jana katika uzinduzi huo vikundi vinne vitafanya maonesho ya sanaa ya ngoma za asili na sarakasi.
Alivitaja vikundi hivyo kuwa ni Dragon Acrobatic group, Happy Centre, Shule ya sèkondari ya Hazina na kikundi cha ngoma za asili cha Mlonge Culture troup.
Alisema mbali ya kutambulisha sarakasi kwa jamii pia itatoa nafasi kwa vijana wanaotaka kujifunza mchezo huo kujiandikisha na kupewa mafunzo ya sarakasi katika vikundi hivyo.
Mwenyekiti Pembe alisema maandalizi ya onesho hilo yamekamilika na mabalozi wa nchi mbalimbali wamealikwa kitaanza saa 12 jioni hadi saa 3 usiku kiingilio ni bure.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇