LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 25, 2022

BILIONI 1.8 KUJENGA VITUO VITANO VYA CHUO KIKUU


Na WyEST

Mwanza 


Serikali imetoa shilingi Bilioni 1.8 kwa ajili ya kujenga vituo vya Chuo Kikuu Huria katika Mikoa Mitano Nchini .


Hayo yameelezwa na  

Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wakati akizungumza katika Mahafali ya  41 Chuo hicho yaliyofanyika jijini Mwanza. 


Ameitaja Mikoa itakayonufaika kuwa ni Geita, Kigoma, Lindi, Simiyu na Manyara ambapo katika mikoa hiyo vituo vinatumia majengo ya kukodi na hivyo kuongeza gharama ya uendeshaji.


Mkenda ameongeza kuwa Chuo Kikuu Huria pia kimetengewa fedha kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) kwa ajili ya  ujenzi wa miundo mbinu ikiwemo maabara , kusomesha wahadhiri na miradi mingine.


"Serikali kwa kutambua mchango wa Chuo  Kikuu Huria katika kupeleka elimu kwa jamii kupitia mradi wa HEET tutajenga maabara saba katika mikoa ya Njombe, Arusha, Dodoma, Mwanza, Kigoma, Mtwara na Pwani ambazo zitajikita katika tafiti za kisayansi kulingana na shughuli na mahitaji muhimu ya eneo husika," amefafanua Waziri Mkenda.


Zaidi ya Wahitimu 4,000 wametunukiwa Shahada mbalimbali zikiwemo Shahada Umahiri na Uzamivu wakiwemo wanafunzi kutoka nchi jirani za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ghana, Malawi, Zambia, Congo, Namibia na Ethiopia.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages