LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 26, 2022

AMIRI JESHI MKUU RAIS SAMIA ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WANAFUNZI 724 CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI JIJINI ARUSHA, LEO

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Samia Suluhu Hassan, akikagua Gwaride la Heshima kabla ya Kuwatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 724 (Wanaume 635) (Wanawake 89) kwa Cheo cha Luteni Usu, katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha, leo.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Samia Suluhu Hassan, akipokea Wimbo wa Taifa na wa Afrika Mashariki kabla ya kukagua gwaride la heshima na Kutunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 724 (Wanaume 635) (Wanawake 89) kwa Cheo cha Luteni Usu katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha, leo.

Kisha, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Samia Suluhu Hassan, akawakabidhi zawadi Maafisa Wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo yao kabla ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa 724 Wanafunzi, katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha, leo.👇

=========

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Samia Suluhu Hassan, akiwatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 724 (Wanaume 635) (Wanawake 89) kwa Cheo cha Luteni Usu katika Sherehe zilizofanyika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) Mkoani Arusha, leo.

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Samia Suluhu Hassan, akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Wanafunzi mara baada ya Kuwatunuku Kamisheni kwa Cheo cha Luteni Usu kwenye Sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani, leo.
Wahitimu
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Samia Suluhu Hassan, akiwatunuku Shahada ya Sayansi ya Kijeshi Wahitimu 109 kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha kwa kushirikiana na Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) kwenye Sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha, leo.
Baadhi ya Viongozi mbalimbali, Wakuu wa Majeshi Wastaafu, Maafisa wa Juu kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa kwenye Sherehe za Kamisheni kwenye Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha, leo.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Samia Suluhu Hassan, akiwapa zawadi Wahitimu waliofanya vizuri kwenye masomo yao ya Shahada ya Sayansi ya Kijeshi kwenye Sherehe za Mahafali zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha, leo.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Samia Suluhu Hassan, akifunga Sherehe za Mahafali ya wahitimu hao, zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha, leo.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na Wahitimu wa Shahada ya Sayansi ya Kijeshi kwenye Sherehe za Mahafali zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha, leo.

 ©Nov. 2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages