Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Temeke
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, umekamilisha safu zote za Uongozi kufuatia kupata Wajumbe wake sita wa Kamati ya Utekelezaji katika Uchaguzi uliofanyika katika Mkutano wa Baraza Kuu uliofanyika katika ukumbi wa Iddi Nyundo wilayani humo, jana, Oktoba 28, 2022.
Wajumbe sita wa Kamati ya Utekelezaji waliopatikana kutokana na Wajumbe wanane wa Baraza la UWT wilayani humo, baada ya Uchaguzi huo uliofanyika kwa utulivu mkubwa ni Gladis Haule, Elizabeth Tossy, Hawa Madenge, Mary Maduhu, Subira Kingo na Fatuma Mbottoni huku Zainabu Selemani na Mwajuma Kisengo wakibaki baada ya kuwa wa mwisho ka wingi wa kura.
Akizungumza baada ya washindi kutangazwa, Mwenyekiti wa UWT Temeke Lawama Mikidadi aliwakumbusha Wanachama wote wa UWT wilayani humo, walioshiriki katika Chaguzi za ngazi mbalimbali kusahau 'maumivu' ya chaguzi hizo na badala yake waendelee kuwa kitu kimoja hadi kukifanya Chama Cha Mapiduzi (CCM) na UWT kuwa imara zaidi.
"Hiki tulichofanya leo ndiyo Kikao cha kwanza tangu tufanye Uchaguzi wa viongozi ngazi zote katika Jumuiya yetu hapa Temeke, sasa kwa kuwa leo tumekamilisha safu zote, sasa nawakumbusha tena ndugu wanachama na viongozi kwamba uchaguzi umekwisha, wote tusahau 'maumivu' yaliyotokana na uchaguzi", akasema Lawama na kuongeza;
"Inatupasa kusahau tofauti zetu zilizokuwepo wakati wa Uchaguzi kwa kuwa sasa kazi iliyopo mbele yetu ni kuwa bega kwa bega katika kumuunga mkono Mwenyekiti wa Chama chetu, Rais Samia Suluhu Hassan, katika kukiimarisha Chama na kuwatumikia Wananchi kwa bidii zaidi".
Mkutano huo wa Baraza Kuu ulihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali Waalikwa wakiwemo Mwenyekiti wa CCM Temeke Zena Mgaya, Katibu wa CCM Temeke Kite Mfilinge, Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Samwel Kiogolo ambao kwa nyakati tofauti walipata nafasi ya kuzunumza na wajumbe wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa UWT Temeke Lawama Mikidadi akizungumza baada ya kutangazwa matokeo ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT wilaya hiyo, wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu uliofanyika leo katika Ukumbu wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Zena Mgaya.
Picha hatua kwa hatua hadi mwisho wa Mkutano huo 👇
Wajumbe wakijimwayamwaya ukubini kabla ya Viongozi kungia ukumbini.Wajumbe wakiendelea kujjimwayamwaya ukubini kabla ya Viongozi kungia ukumbini.
Wajumbe wakiwa wamesimama wakati Mwenyekiti wa UWT Temeke Ndugu Lawama akiingia ukumbini na msafara wake. |
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Temeke Lawama Mikidadi akiwa amewasili ukumbini katika Mkutano wa Baraza Kuu la UWT wilaya hiyo, uliofanyika katika Ukumbu wa Iddi Nyundo, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Katibu wa UWT Temeke Jane Chatanda.kwenyekiti wa UWT Wilaya ya Temeke Lawama Mikidadi akiwa ameketi na kuanza kusawazisha mambo fulani baada ya kuwasili ukumbini katika Mkutano wa Baraza Kuu la UWT wilaya hiyo, uliofanyika katika Ukumbu wa Iddi Nyundo, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Katibu wa UWT Temeke Jane Chatanda.kk
Wajumbe wakiwa wameketi kusubiri muongozo wa Mwenyekiti.
Wajumbe wakiwa wameketi ukumbini kusubiri muongozo wa MwenyekitiMkurugenzi wa Uchaguzi katika Kikao hicho, Katibu wa UWT Temeke Jane Chatanda akitoa utambulisho na muongozo wa shughuli nzima ya kikao hicho. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Zena Mgaya na Mweneyekiti wa UWT Wilaya hiyo Lawama Mikidadi.
Madiwani wa Kata mbalimbali na Viti Maalum ambao ni Wajumbe wa Mkutano huo wakiwa ukumbini.Wagombea wakiwa wameketi eneo Maalum katika Mkutano huo.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Temeke Lawama Kikidadi, akizungumza na kufungua Mkutano huo wa Baraza Kuu.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Temeke Lawama Kikidadi, akifafanua jambo wakati akizungumza na kufungua Mkutano huo wa Baraza Kuu. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Zena Mgaya. |
Wagombea wanane wa nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utekelezaji wakiwa na karatasi zenye namba za utambulisho wao wa kuombea kura kwa wajumbe.
Wajumbe wakipiga kura.
Kijana wa UVCCM akikusanya kura.
Wagombea wakikisimamia wakati kura zao zikihesabiwa.
Mkurugenzi wa Uchaguzi huo Katibu wa UWT Temeke Jane Chatanda akitangaza matokeo.
Matokeo yenyewe ndiyo hayo👆. Wagombea wote wakiwa wameyatia saini zao kuashiria kuyakubali.
Wagombea waliochaguliwa wakiwa wamesimama baada ya kutangazwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Temeke Lawama Mikidadi akimpatia cheti aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT Wilaya hiyo ambaye kwa sasa ni Diwani, Mariyamu Mtemvu kwa kutambua mchango wake katika UWT Wilaya hiyo.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Temeke Lawama Mikidadi akimpatia cheti na zawadi za saa na sare ya CCM, Katibu wa CCM Wilaya ya Temeke Komredi Katibu wa CCM Temeke Kite Mfilinge, kutambua mchango wake kwa UWT Wilaya hiyo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Temeke Komredi Kite Mfilinge akizungumza kutoa nasaha kwa UWT na kutoa shukurani kwa zawadi alizopewa kutambua mchango wake kwa Chama na UWT.Mwenyekiti wa CCM Temeke Zena Mgaya akizungumza kuwafuda UWT mwishoni mwishoni mwa Mkutano huo wa Baraza Kuu.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Temeke Lawama Mikidadi akitoa hotuba yake ya kufunga Mkutano huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇