Na Mwandishi Maalum, Dodoma
Jamhuri ya Muungano waTanzania imeombwa kuridhia baadhi ya itifaki za mabadiliko ya Mkataba wa Kimataifa wa Ulinzi wa Nyezo za Nyukilia (Convention on the Physical Protection of Nuclear Material).
Taarifa iliyoandaliwa na kutolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Maura Mwingira, imesema Ombi hilo limetolewa leo Oktoba 26, 2022, na Bw.Richard Sseggane kutoka Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomu Duniani( IAEA), Ujumbe kutoka IAEA ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania Prof. Lazaro Busagali ulipoitembelea Ofisiya Mwanasheria Mkuu wa Serikali jijini Dodoma na kufanya mazungumzo na Mwandishi Mkuu wa Sheria Bw. Onorius Njole.
Taarifa hiyo imesema, Bw. Sseggane amebainisha kwa kueleza kwamba, ingawa Tanzania imeridhia Mkataba huo, (The Convention on the Physical Protection of Nuclear Material) akini bado haijaridhia baadhi ya itifaki za mabadiliko ya mkataba huo, hivyo basi, wanaiomba Tanzania, kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikalia mbayo ni mdau mkubwa katika mchakato wa uridhiaji wa mikataba ya kimataifa kusaidia.
“Tunaiomba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iendelee kushirikiana na Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania na Wizara husika katika kufanikisha kuridhiwa kwa Itifaki zilizobakia”, akasihi Bw. Richard Sseggane kutoka IAEA.
Taarifa hiyi imeongeza kwamba, Ujumbe huo pamoja na kuzungumzia kuhusu Mkataba huo pia alizungumzia mkataba mwingine wa Kimataifa wa Utokomezaji wa Vitendo vya Ugaidi wa Nyukilia (the International Convetion for Suppression of Acts of Nuclear Terrorism).
Aidha Ujumbe huo umeishukuru Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuendelea kuwa mdau muhimu katika wa masuala ya Nguvu za Atomu hususani katika eneo la maboresho ya sheria.
"Kwa upande wake, Mwandishi Mkuu wa Sheria Bw. Onorius Njole aliyekuwa mwenyeji wa Ujumbe huo kwa niaba ya Naibu Mwanasheria Mkuuwa Serikali, ameuhakikisha Ujumbe huo kwamba, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali itakuwa tayari kutoa ushirikiano wowote utakaohitajika katika eneo hilo", imesema taarifa hiyo na kuongeza;
Aidha Mwandishi Mkuu wa Sheria ameushukuru Ujumbe huo kwa kutoa maelezo ya kina uhusu Mikataba hiyo ya Kimataifa lakini pia kwa kuitembelea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kutambua nafasi ya Mwanasheria Mkuuwa Serikali katika masuala yote yanayohusu mikataba ya Kimataifa.
Bw. Onorius Njole alitumia fursa hiyo kuelezea majukumu mbalimbali ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yakiwamo ya mapitio ya sheria mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa pamoja na mchakato wa kuzitafsri sheria hizo katika lugha ya Kiswahili.
Mwandishi Mkuu wa Sheria Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Onorius Njole (Wanne kushoto) akiwa na Ujumbe kutoka Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomu Duniani (IAEA pamoja na Ujumbe wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania ukiongozwa na Profesa Lazaro Busagala wakati Ujumbe huo ulipoitembelea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jijini Dodoma, leo Oktoba 26, 2022. (Picha na Ofisi ya CAG).
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇