LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 2, 2022

SHAKA: BAADA YA UCHAGUZI NDANI YA CCM VIONGOZI WOTE WAPYA WATAPEWA MAFUNZO

Dimani, Zanzibar

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema Chama kimeona umuhimu wa kuwajengea uwezo viongozi wote wapya ndani ya Chama na kwamba baada ya Kukamilika kwa Uchaguzi unaondelea kote nchini watapatiwa mafunzo ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi.


Aidha, amesema CCM bado ni eneo muhimu katika kuzalisha viongozi bora na tegemeo kwa maendeleo ya nchi.


Shaka ameyasema hayo aliposhiriki mkutano mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa CCM Wilaya ya Dimani, Mkoa wa Mjini Magharibi ambao umefanyika leo Oktoba 2, 2022.


Asema viongozi wanapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia mipaka kulingana na Katiba ya CCM, kanuni na miongozo ya Chama, hivyo ili kwenda sawasawa ni lazima kuishi katika misingi ya Katiba, kanuni na taratibu.


"Wengi tuliopo hapa ni viongozi wapya, tumekabidhiwa dhamana hii muhimu ya uongozi, Chama kimeweka mpango maalumu, ndani ya muda mfupi ujao wa kuwapatia semina viongozi katika ngazi zote," amesema Shaka.

Shaka akipiga kura Kwenye Uchaguzi huo.




No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages