LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 15, 2022

NDEJEMBI: MSITUMIE FEDHA ZA MKOPO WA HATIMILIKI ARDHI, KUOLEA MKE WA PILI, KUTUMBUA RAHA+video


Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deo Ndejembi amewaasa wananchi kuacha tabia ya kutumia fedha za mkopo unaotokana na dhamana ya hatimiliki ardhi kuolea mke wa pili na kwenda mjini kutumbua raha.


"Mkitumia fedha hizo za mkopo zikaisha, taasisi za fedha mlikokopa zitakuja kutaifisha mashamba yenu,"Ndejembi.


Ndejembi ametoa onyo hilo alipokuwa akihutubia baada ya kuzindua jengo la masijala lililojengwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) katika Kijiji cha Nakalonji, Kata ya Mbondo wilayani Nachingwea Oktoba 12, 2022.

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa MKURABITA, Mujungu Masyenene akiwasalimia wananchi wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi huo.


 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Naibu Waziri Ndejembi akiwaasa wananchi kuhusu matumizi ya mkopo...

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages