LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 15, 2022

BENKI YA DUNIA YAIMWAGIA SIFA TANZANIA KWA UCHUMI IMARA


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Taufila Nyamadzabo, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania, unaoongozwa na Mhe. Dkt. Nchemba, kwenye Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) kushoto) akizugumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Taufila Nyamadzabo (hayupo pichani), walipokutana na kufanya mazungumzo, kwenye Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Jijini Washington D.C, nchini Marekani. Kulia kwake ni Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Rished Bade, na Afisa anayesimamia Dawati la Benki ya Dunia kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Peter Masolwa

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kulia) akizugumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Taufila Nyamadzabo (hayupo pichani), walipokutana na kufanya mazungumzo, kwenye Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Jijini Washington D.C, nchini Marekani. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil na wa tatu kulia ni Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Rished Bade na Ofisa anayesimamia Dawati la Benki ya Dunia, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.Peter Masolwa.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), akizugumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Taufila Nyamadzabo (hayupo pichani), walipokutana na kufanya mazungumzo, kwenye Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Jijini Washington D.C, nchini Marekani. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil na kushoto ni Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Rished Bade na Ofisa anayesimamia Dawati la Benki ya Dunia, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Peter Masolwa.


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), akizugumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Taufila Nyamadzabo (hayupo pichani), walipokutana na kufanya mazungumzo, kwenye Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Jijini Washington D.C, nchini Marekani. Kulia ni Mwambata wa Uchumi (ubalozi wa Tanzania nchini Marekani), Bw. Said Nyange, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil na kuklia kwa Mhe. Dkt. Nchemba ni Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Rished Bade na Ofisa anayesimamia Dawati la Benki ya Dunia, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Peter Masolwa.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango-Washington D.C, Marekani)
……………………………………..
Na Benny Mwaipaja, Washington D.C, Marekani
BENKI ya Dunia imeimwagia sifa Tanzania kwa usimamizi mzuri wa uchumi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayopata fedha kutoka kwenye taasisi hiyo ikilinganishwa na nchi nyingine nyingi za Afrika.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Taufila Nyamadzabo, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania, unaoongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kwenye Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Dkt. Nyamadzabo alisema kuwa Tanzania ni nchi ya mfano katika usimamizi wa uchumi ambapo licha ya majanga ikiwemo changamoto za UVIKO 19 na vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraine, tathimini inaonesha kuwa uchumi wa Tanzania uko imara na nchi inakopesheka.
Aliahidi kuwa Benki yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kukuza uchumi na kuwaondolea umasikini wananchi wake kwa kusaidia rasilimali fedha zitakazotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alimweleza Mkurugenzi huyo Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika, Dkt. Taufila Nyamadzabo kwamba uchumi wa Tanzania unazidi kuimarika na kwamba Serikali itaendelea kuchukua hatua muhimu kuhakikisha uchumi unazidi kuimarika na kuleta ahueni kwa wananchi.
Alifafanua kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2022/2023 uchumi umekua kwa asilimia 5.4 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 5.0 katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha uliotangulia 2021/2022 na kwamba kutokana na mipango kabambe iliyowekwa na Serikali uchumi utakua zaidi hadi kufikia wastani wa asiliia 6.3.
Aidha, Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alirejea shukrani zake kwa Benki ya Dunia kwa kuitengea Tanzania jumla ya dola za Marekani bilioni 2.1 sawa na shilingi trilioni 4.9 katika mzunguko wa 20 wa IDA (Julai 2022 – Juni 2025) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi pamoja na kupunguza umasikini wa watu wake.
Mpaka sasa Benki ya Dunia imewekeza zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 7.2, sawa na takriban shilingi za Tanzania trilioni 16.7 kwa ajili ya kutekeleza miradi zaidi ya 29 nchini Tanzania ambapo kati ya miradi hiyo, 24 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 6.41 ni ya kitaifa na mingine 5 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 0.75 ni ya kikanda.








No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages