Takwimu.muhimu za Ziwa Victoria:
*Umri: takribani miaka 400,000
*Ujazo wa maji: takriban 2,424 cubic kilometers
*Jumla ya aina ya samaki (fish species): zaidi ya 500.
Samaki wamepungua sana kwa hiyo umamuzi wa Serikali wa kutoa MIKOPO ISIYOKUWA na RIBA, ni uamuzi mzuri sana. Kwani mikopo hiyo itaenda kubadili mitindo ya uvuvi ndani ya Ziwa hilo.
Muhimu sana ni kuanzishwa kwa UVUVI wa VIZIMBA (cage fish farming, aquaculture) ambao ni wa kisasa na wenye uvunaji mkubwa wa samaki.
Wavuvi wa Jimbo la Musoma Vijijini, wenye uzoefu mkubwa wa uvuvi wamejitokeza kwa wingi kuomba mikopo hiyo ya kutoka Serikalini.
Shukrani nyingi sana zimetolewa kwa Serikali yetu. Tafadhali sikiliza CLIPS/VIDEO 2 zilizoambatanishwa hapa
Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Alhamisi, 20.10.2022
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇