Na Bashir Nkoromo, Kigamboni
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kigamboni Stanley Mkandawile amewataka waliochaguliwa katika Uchaguzi wa CCM katika Wilaya hiyo, kujiepusha kuisema vibaya mitaani Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, badala yake waitee kwa kuyasema mazuri yake.
Mkandawile amesema, siyo kwamba Serikali haipaswi kusemwa watendaji katika nafasi za kuchaguliwa, kuteuliwa au kuajiriwa na Serikali wanapofanya vibaya, lakini kusemwa huko hakufanywi mitaani na viongozi wa CCM, kwa sababu wanayo nafasi ya kuonya au kuchukua hatua dhidi ya watendaji wabovu kupitia vikao vya Kikatiba vya Chama katika ngazi wanazohusika.
"Njoja hili nilifafanue kidogo, mnajua, kama Mbunge au Diwani wa CCM akifanya mabaya mnapoisema Serikali, watu wengine wanaona kwamba CCM yote ni mbaya, sasa hii ni haifai, kwa sababu wakati wa uchaguzi hata kama Mbunge huyo au diwani aliyehusika hatagombea, yule atakayeuliwa na CCM kugombea naye ataonekana hafai kwa kuwa anatoka CCM ile ile, kwa hiyo CCM italikosa Kata au jimbo wakati inahitaji sana kushinda.
Unachotakiwa kufanya Kiongozi wa CCM, ni kulipeleka kosa la Mbunge au Diwani kwenye Vikao vya Kikatiba vya Chama ambavyo kwa mamlaka ambayo vikao hivyo vinayo, vitamuita kuzungumza naye na vikiridhika kwamba ni kweli na siyo umbea wa mitaani tu, vitamchukulia hatua stahiki", akasema Mkandawile na kuongeza;
"Ninyi Viongozi wa CCM, moja ya jukumu Muhimu ukiacha lile la kusimamia utendaji wa Serikali katika ngazi mlizomo, sasa ni hili la kuisemea Serikali mazuri inayofanya, na hili siyo la kuisemea kwenye vikao tu, ni mahali popote unapokuwa hata kwenye vibanda vya kawahawa.
Na hili la kuisemea Serikali kwako wewe kiongozi wa CCM siyo jambo gumu, maana kama wewe ni kiongozi madhubuti lazima uwe unayajua mema na mazuri yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa na Serikali ya Chama chako maana unayo nafasi ya kuyajua.
Kwa mfano, ninyi mliochaguliwa leo, hivi kweli mtakuwa hanyajui mazuri yaliyofanywa na yanayoendelea kufanya na Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Mwenyekiti wetu wa Chama Rais Samia? Hizi Barabara za lami zilizojengwa na zinazoendelea kujengwa hamzijui? au ninyi Ujenzi wa madarasa ya shule na mambo tele yanayofanywa na Serikali hamuoni kwenye Kata zenu?".
Mkandawile akasema, licha ya kwamba Chama katika Wilaya hiyo ya Kigamboni kinaamini kuwa waliochaguliwa ni viongozi safi na wenye weledi wa uongozi, lakini baadaye kitaandaa makongamano maalum kwa ajili kutoa mafunzo elekezi hasa kwa wale ambao ni wapya kabisa.
Katika Uchaguzi huo ambao ulifanyika jana, katika Ukumbi wa Chuo cha Mwalaimu Nyerere, Kivukoni aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Yahya Sikunjema aliibuka mshindi na kutangazwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM Wilaya ya Kigamboni baada ya kupata kura 277 dhidi ya Mwenyekiti wa UVCCM aliyemaliza muda wake Mponela Matei aliyepata kura 174 na Mwanamama Maimuna Yussuf aliyepata kura moja.
Wengine walioghara katika Uchaguzi huo ni Waliofaulu kuwa Wawakilishi wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Robert Malangila aliyepataaliyepata kura 386, Dotto Msawa kura 364 na Asha Feruzi aliyepata kura 237.
Nafasi nyingine zilikuwa ni nafasi wawakilishi UWT nafasi 4 ambapo waligombea 12, Wawakilishi Wazazi nafasi 2 ambapo waligombea 6, na UVCC nafasi nne ambapo waligombea 11.
Matokeo yalitangzwa na Msimamizi w Uchaguzi huo, Mjumbe wa Halmanashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Dk. Fenela Mkangala.
Mkanda Kamili wa picha za Uchaguzi huo👇
Mwenyekiti Sikunjema akizungumza baada ya kupewa kiti meza kuu, " Sasa Uchaguzi umeisha, nitaongoza kwa Mujibu wa Katiba yetu ya CCM, Sasa wale wote mliokuwa wapigadebe wangu mwisho ni hapa, Uchaguzi umeisha. Usije ukasema Ohh, Sikunjema ninamuweza, hiyo kwangu hakuna wote nitawatendea sawa." akasema Sikunjema. Kushoto ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi huo Katibu Stanley Mkandawile."Mimi Mponela Matei nimepokea matokeo kwa mikono mwili, sina kinyongo. namuomba Kama Mwenyekiti alivyosema, Uchaguzi umeisha, sasa CCM Kigamboni tuendelee kuwa kitu kimoja, hakuna makundi tena na wala mimi sina kundi. Asanteni woote mlinipa kura", akasema, Matei wakati akitoa neno baada ya kuitwa na Mwenyekiti Sikunjema.
"Yaani huyo Mkandawile (kushoto) Wanakigamboni mmepata jembe, namjua tangu tukiwa UVCCM, ni mchapakazi kweli kweli, tumpe ushirikiano", akasema Sikunjema wakati akiendelea kuzungumza baada ya kukaa meza kuu. Watatu kulia ni Kamisaa wa CCM, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa.
Mkandawile alipokuwa akimkaribisha Sikunjema kuja meza kuu
"Bosi karibu sana" akasema Mkandawile baada ya Sikunjema kufika meza kuu akishangiliwa na wajumbe.
Kisha wakakumbatiana kwa furaha.
Mwenyekiti aliyeondoka akampongeza Sikunjema kabla ya kuondoka meza kuu kumpisha kiti.
Woooote ukumbi wakashangilia wakati Mwenyekiti aliyeondoka akiwa amemkaribisha Sikunjema kuchukua nafasi yake.
Mkandawile akizungumza kumwita Sikunjema meza Kuu baada ya kuchaguliwa
Waliofaulu kuwa Wawakilishi wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Robert Malangila aliyepataaliyepata kura 386, Dotto Msawa kura 364 na Asha Feruzi aliyepata kura 237,Wajumbe wakishangiliwa Sikunjema alipotangzwa kuwa mshindi.
Sikunjema akiwa amebebwa na baadhi ya Wajumbe alipotangazwa kuwa mshindi.
Sikunjema akipongezwa na Mponela.
Msimamizi wa Uchaguzi huo Dk. Fenela alipokuwa akitangaza matokeo.
Mwenyekiti wa muda alipokuwa akimualika Msimamizi wa Uchaguzi huo kutangaza matokeo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Kigamboni Ashura Kizigo akiaga kwenye Uchaguzi huo, kufuatia kuteuliwa kuwa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Manyara. akaahidi kuandaa Royol Tour ya mkoa wa Manyara na Kigamboni.
Katibu Mkandawile alipokuwa akiwasindikiza Wazee wa CCM waliohudhuria kikao hicho, wakati wakiondoka.
Msimamizi wa Uchaguzi huo Dk. Fenela alipokuwa akiwaonyesha kura zao baadhi ya kundi la wagombea, wakati wa kuhesabu kura.
Msimamizi wa Uchaguzi huo Dk. Fenela alipokuwa akitoka na jopo lake kuhesabu kura za nafasi ya Mwenyekiti.
Wajumbe walipokuwa wakipiga kura kuchagua moja ya nafasi za wagombea.
Mwanadada Winfrida Shonde alipokuwa akiomba kura kwa wajumbe. Alifanikiwa kupata nafasi ya kushinda nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kigamboni, kundi la UWT.
Mgombea wa nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kigamboni, kundi la UWT Linda Mbwiliza akiomba kura kwa wajumbe ili kupata nafasi hiyo. Hata hivyo kura hazikutosha.Matei alipokuwa akiomba kura kuwanaia nafasi ya Uenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni.
Sikunjema alipokuwa akiomba kura kuwanaia nafasi ya Uenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni.Wajumbe wakifuatilia hali ya mambo ukumbini.
Baadhi ya Wajumbe wakikimbilia ukumbini baada ya msimamizi wa Uchaguzi kutishia kufunga mlango muda mfupi kabla ya uchaguzi huo kuanza. Inadaiwa wajumbe hao walikusanyika kundi eneo la Chooni kwa ajili ya kupokea rushwa. ambapo Katibu Mkandawile aliagiza watakaobainika wakamatwe na Takukuru ambao aliwaalika kwenye uchaguzi huo.
Baadhi ya Wajumbe wakikimbilia ukumbini baada ya msimamizi wa Uchaguzi kutishia kufunga mlango muda mfupi kabla ya uchaguzi huo kuanza. Inadaiwa wajumbe hao walikusanyika kundi eneo la Chooni kwa ajili ya kupokea rushwa. ambapo Katibu Mkandawile aliagiza watakaobainika wakamatwe na Takukuru ambao aliwaalika kwenye uchaguzi huo.Badhi ya Wajumbe wakikimbilia ukumbini baada ya msimamizi wa Uchaguzi kutishia kufunga mlango muda mfupi kabla ya uchaguzi huo kuanza. Inadaiwa wajumbe hao walikusanyika kundi eneo la Chooni kwa ajili ya kupokea rushwa. ambapo Katibu Mkandawile aliagiza watakaobainika wakamatwe na Takukuru ambao aliwaalika kwenye uchaguzi huo.Katibu Mkandawile alipokuwa akizungumza kabla ya kikao cha uchaguzi huo kuanza rasmi.
Wajumbe Ukumbini.
Mwenyekiti aliyeondoka Chaula akizungumza ukumbini baada ya kuwasili ukumbini wakati huo akiwa bado hajavua madaraka.
Wajumbe ukumbini.
Kamisaa wa CCM, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa akisalimia baada ya kutambulishwa ukumbini.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake akisalimia baada ya kuwasili ukumbini kabla yajajivua madaraka.
Mwenyekiti Chaula aliyemaliza muda wake akikaribishwa na Katibu Mkandawile baada ya kuwasili ukumbini wakati huo akiwa bado hajavua madaraka yake.
Mwenyekiti Chaula akisalimia alipokuwa akiingia ukumbini kabla ya kujivua madaraka.
Baadhi ya Maofisa wakisubiri kugawa viatmbulishi wa wajumbe na wagombea wakati wa Mkutano huo.
©October 2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇