LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 19, 2022

KAULI TOKA OFISI YA MBUNGE JIMBO LA CHALINZE

 


Kwanza baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema niendelee kuwapongeza tena Wana -Chalinze kwa ushirikiano ambao kila siku umekuwa unaleta Mafanikio katika Mambo mbalimbali ndani ya Halmashauri Yetu.


Siku imekuwa na mazuri na Yanayofikirisha ndani yake. Nimepokea taarifa zinazomuhusu Bint yetu anayeitwa Iptosum Suleiman Slim kuhusu shida iliyotokea kwenye Mitihani yake ya Darasa la Saa katika shule ya Msingi ya Chalinze Modern. Binafsi nieleze kwanza masikitiko kwa tukio zima maana linatupa nafasi ya kuhoji juu ya ukweli wa habari nzima. Si jema kwa Mwanafunzi, Shule wala Halmashauri yetu ya Chalinze. 


Asubuhi nimeuelekeza Uongozi wa Halmashauri yetu na Shule kutafuta jawabu ya changamoto hii. Nimewataka kuhakikiaha jamii inapatiwa taarifa za ukweli kuhusu tukio zima na kama itakuwa kuna yeyote aliyehusika kuweka mazingira haya ikiwa ni dhuruma kwa mwanafunzi wetu huyu au kuchafua sura ya Shule yetu basi hatua za msingi kupata haki zifuate. 


Elimu ni kipaumbele chetu,kusomesha watoto wa kike ndiyo njia ya ukombozi wetu. Ninaamini Halmashauri yetu yenye wajibu wa kusimamia Elimu watatoa taarifa punde kama nilivyoelekeza. 


Tunaomba Utulivu wakati jambo hili linafanyiwa kazi hili tupate muafaka wake. Ninaamini Haki itatendek kwa pande zote 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages